Kwa mujibu wa taarifa ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatollah Sheikh Bashir Hussein Najafi, mmoja wa Marja‘ wa Najaf Ashraf, wakati wa mapokezi ya mazuwari kutoka Iran, alisisitiza juu ya umuhimu wa kujitenga na maadui wa Uislamu, na maadui wa Mtume na Ahlul-Bayt wake watoharifu (aa), na akataja ziara ya Atabati Tukufu nchini Iraq kuwa ni miongoni mwa neema kubwa za Mwenyezi Mungu.
Mazuwari hao walikuwa wametoka katika mikoa kadhaa ya Iran, jambo linaloashiria kina cha uhusiano wa kiroho na kihisia kati ya waumini na Marja‘iyya.
Katika kikao hichi, Mtukufu Ayatollah, alisisitiza kuwa ziara ya Atabati Tukufu nchini Iraq ni moja ya neema kubwa za Mwenyezi Mungu, na akatoa wito wa kudumu katika njia ya haki na ukweli, pamoja na kujitenga na maadui wa Uislamu, Mtume Mtukufu na kizazi chake kitoharifu (as).
Mtukufu Ayatollah Bashir Hussein Najafi, pia alitoa nasaha na maelekezo ya kidini na ya kindugu kwa mazuwari hao, na akasisitiza juu ya umuhimu wa kushikamana na kuendelezaa mwenendo wa Imam Hussein Shahīd (as), kwa kuwa jambo hili lina athari kubwa katika kuisafisha nafsi na kuimarisha imani.
Mwishoni mwa kikao hicho, Mtukufu Ayatollah alimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awalinde waumini, awalinde dhidi ya hila na njama za wahaini, na awaongoze katika kufuata njia ya Ahlul-Bayt (as) katika itikadi na matendo.
Maoni yako