Alhamisi 28 Agosti 2025 - 18:49
Umoja wa Waafrika Qum Irani, wakutana na Mwakilishi wa Kwanza wa Kiongozi wa Mapinduzi katika Bara la Afrika

Hawza/ Raisi wa Umoja wa Waafrika waliopo Qum nchini Irani, leo hii siku Alkhamisi akiongozana na ujumbe wake maalumu, wamekutana na Hujatul Islam sheikh Mahdawi Puur, Mwakilishi wa kwanza wa Kiongozi wa mapinduzi katika masuala ya kidini Barani la Afrika

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa  Shirika la Habari la Hawza, kikao hicho kilicho kuwa na anuani ya "kufahamiana na kutambulishana" kimefanyika leo hii tareh 28/8/2025 Qum nchini Iran, huku kikihudhuriwa jopo la wanazuoni wasiopungua 30, katika kikao hicho baada ya kufunguliwa kwa kisomo cha Qur'ani kisha Raisi wa Umoja wa Waafrika nchini Iran Dkt. Muhammad Amiin Sajo, alitoa shukrani zake na hatimaye kuutambulisha ujumbe ambao alikuwa ameambatana nao, na baada ya hapo alimuachia nafasi naibu wake Dk. Abuubakar Salat, ambae alieleza kwa kina historia kamili ya umoja huo pamoja na harakati ambazo umoja huo umekuwa ukizifanya hapa Iran na nje ya Iran, na hatimae akagusia changamoto mbali mbali ambazo umoja huo umekuwa ukikumbana nazo.

Hujjatul islam walmuslimin Sheikh Mahdawi Pur, Mwakilishi wa kwanza wa kiongozi wa Mapinduzi Barani Afrika katika mas-ala ya sheria, nae pia alipata nafasi ya kuzungumza katika kikao hicho, katika hutuba yake, alianza na utambulisho wake pamoja na jopo lake, kisha akaelezea tajruba aliyokuwa nayo katika utendaji kazi, ambapo aliashiria kwamba alikuwa ni mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi nchini India kwa takriban miaka 15, na hatimae kwa sasa anajisikia fakhari kupata nafasi ya kuwahudumia Waafrika.

Katika kina cha mazungumzo yake alianza na kuelezea kisa cha mwanfunzi ambae alihitimu masomo yake lakini kutokana na ugumu wa maisha ikambidi aende kuonana na Ayatullh Bahjat (ra) ili kumtaka ushauri, Ayatullah Bahjat alimuambia yule mwanazuoni kwamba wewe nenda ukafanye tableegh, mimi nakukabidhi kwa Mwenyezi Mungu na vile vile Mwenyezi Mungu namkabidhi kwako, katika kulielezea hilo alisema kwamba; Kumkabidhi Mwenyezi Mungu kwake ni kuikabidhi dini ya Mwenyezi Mungu, alisema; mwanazuoni siku zote yampasa kufahamu kwamba dini ya Mwenyezi Mungu ipo kwenye himaya yake, yeye ndie mwenye dhima ya kuyafikisha mafunzo sahihi yanayo hitajika katika dini, huku ndio kumkabidhi Mwenyezi Mungu kwake.

Katika muendelezo wa mazungumzo yake pia aligusia wadhifa aliokuwa nao mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi katika mas-ala ya kisheria, na hatimae pia aligusia nukta ya umoja na mshikamo na kuisisitiza kwa kina.

Mwisho wa kikao hicho washiriki walipata nafasi ya kuuliza maswali mbali mbali na hatimae kuweza kujumuika kwa pamoja katika swala ya Adhuhuri.

Umoja wa Waafrika Qum Irani, wakutana na Mwakilishi wa Kwanza wa Kiongozi wa Mapinduzi katika Bara la Afrika

Umoja wa Waafrika Qum Irani, wakutana na Mwakilishi wa Kwanza wa Kiongozi wa Mapinduzi katika Bara la Afrika

Umoja wa Waafrika Qum Irani, wakutana na Mwakilishi wa Kwanza wa Kiongozi wa Mapinduzi katika Bara la Afrika

Umoja wa Waafrika Qum Irani, wakutana na Mwakilishi wa Kwanza wa Kiongozi wa Mapinduzi katika Bara la Afrika

Umoja wa Waafrika Qum Irani, wakutana na Mwakilishi wa Kwanza wa Kiongozi wa Mapinduzi katika Bara la Afrika

Umoja wa Waafrika Qum Irani, wakutana na Mwakilishi wa Kwanza wa Kiongozi wa Mapinduzi katika Bara la Afrika

Umoja wa Waafrika Qum Irani, wakutana na Mwakilishi wa Kwanza wa Kiongozi wa Mapinduzi katika Bara la Afrika

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha