Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjuna ya Shirika la Habari la Hawza, baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji, Mheshimiwa Maxime Prévot, siku ya Jumanne katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutangaza kwamba Ubelgiji imeitambua rasmi Serikali ya Palestina, na baada ya Australia, Uingereza, Kanada na Ufaransa kuongeza shinikizo dhidi ya Israel, maafisa wa utawala huo walionyesha hasira kuhusu tukio hilo
Ubelgiji imetangaza kwamba uamuzi huu umechukuliwa kutokana na kuzingatia janga la kibinadamu linaloendelea kutokea huko Ghaza, na ni jibu kuhusiana na ukiukwaji wa sheria za kimataifa unaofanywa na Israel.
Wataalamu pia wameliona jambo hilo kuwa ni miongoni mwa matokeo ya kutoridhishwa na kitendo cha Israel cha kutwaa ardhi na nchi zaidi.
Baada ya Kanada pia kutangaza kwamba inakusudia kulitambua rasmi taifa la Palestina, ilikabiliwa na ukosoaji wa wazi kutoka kwa Rais wa Marekani, Ikulu ya White House pia haikutoa jibu lolote kwa ombi la shirika la habari la Reuters kuhusu kuchukua msimamo juu ya hatua hii ya Ubelgiji.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya katika kikao chao cha hivi karibuni kilichofanyika mjini Copenhagen waligawanyika katika makundi mawili: kundi moja lilitaka vikwazo na shinikizo kali la kisiasa dhidi ya Israel, ilhali kundi jingine lilipinga kabisa jambo hilo.
Chanzo: Reuters
Maoni yako