Ijumaa 13 Juni 2025 - 14:53
Kurudi kwa Mitume, Maimamu na Waumini wa kweli

Hawza/ Kwa mujibu wa hadithi, Mitume, Maimamu watoharifu (as), na waumini wa kweli – katika zama za "raj‘a" – watarudi tena duniani.

Shirika la Habari la Hawza | Kwa mujibu wa riwaya, Mitume, Maimamu watoharifu (as), pamoja na waumini wa kweli, ni miongoni mwa wale ambao watarudi duniani katika zama za "raj‘a".

Riwaya hizi zinaweza kugawanywa katika makundi manne:

1) Riwaya zinazozungumzia kwa ujumla kurudi kwa Mitume na Maimamu (as)

Imam Swādiq (as) anapofasiri aya isemayo:


"إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِینَ آمَنُوا فِی الْحَیاةِ الدُّنْیا وَیوْمَ یقُومُ الْأَشْهَادُ."

"Hakika Sisi tutawanusuru Mitume wetu na wale waliomuamini, katika uhai wa duniani na siku watakaposimama mashahidi." (Ghāfir: 51),

anasema:

"ذلک والله فی الرجعة، أما علمت أن أنبیاء کثیرة لم ینصروا فی الدنیا وقتلوا والائمة بعدهم قتلوا ولم ینصروا، ذلک فی الرجعة."

Naapa kwa Allah, jambo hili litatimia katika "raj‘a". Je, hujui kuwa Mitume wengi hawakunusuriwa duniani na waliuawa, na hata Maimamu waliokuja baada yao waliuawa na hawakunusuriwa? Hiyo nusura itatokea katika "raj‘a". (Ma‘jam Ahādīth al-Imām al-Mahdi ‘alayhis-salaam, juzuu ya 5, uk. 384)

 2) Riwaya zinazotaja idadi ya Mitume watakaorudi

Imam Swādiq (as) anasema:

"ویقبل الحسین فی أصحابه الذین قتلوا معه ومعه، سبعون نبیا، کما بعثوا مع موسی بن عمران."

Atarudi Imam Husayn (as) pamoja na mashahidi wenzake waliouawa pamoja naye, na atakuwa na Mitume sabini, kama walivyopelekwa pamoja na Mūsā bin ‘Imrān (as). (Ma‘jam Ahādīth al-Imām al-Mahdi ‘alayhis-salaam, juzuu ya 4, uk. 89)

3) Riwaya zinazotaja kwa jina kurudi kwa baadhi ya Mitume na Maimamu (as)

Imam Bāqir (as) anasema:

"وَ إِنَّ دَانِیَالَ وَ یُوشَعَ یَخْرُجَانِ إِلَی أَمِیرِ اَلْمُؤْمِنِینَ یَقُولاَنِ صَدَقَ اَللَّهُ وَ رَسُولُهُ وَ یَبْعَثُ اَللَّهُ مَعَهُمَا إِلَی اَلْبَصْرَةِ سَبْعِینَ رَجُلاً."

Hakika Dāniyāl na Yūsha‘ (as) watafufuliwa na kurejea kwa Amīr al-Mu’minīn (as), na watasema: “Amesema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume Wake,” na Mwenyezi Mungu atawafufua pamoja nao watu sabini kuelekea Basra. (Bihār al-Anwār, juzuu ya 53, uk. 62)

Imam Zayn al-‘Ābidīn (as) naye anasema:

"یرجع إلیکم نبیکم صلی الله علیه وآله وأمیرالمؤمنین علیه‌السلام والائمة علیهم‌السلام."

Watarejeshwa kwenu, Mtume wenu (saw), Amīr al-Mu’minīn (as), na Maimamu (as). (Ma‘jam Ahādīth al-Imām al-Mahdi ‘alayhis-salaam, juzuu ya 5, uk. 327)

Vilevile, Imam Swādiq (as) anasema:

"أَوَّلُ مَنْ یَرْجِعُ إِلَی اَلدُّنْیَا اَلْحُسَیْنُ بْنُ عَلِیٍّ عَلَیْهِ السَّلاَمُ."

Wa kwanza kurejea duniani atakuwa Husayn bin ‘Alī (as). (Bihār al-Anwār, juzuu ya 53, uk. 46)

4) Riwaya zinazoelezea kurudi kwa watu wema kutoka ummah uliopita na kutoka ummah wa Kiislamu

Imam Swādiq (as) amesema:

"یَخْرُجُ اَلْقَائِمُ مِنْ ظَهْرِ اَلْکَعْبَةِ مَعَ سَبْعَةٍ وَعِشْرِینَ رَجُلاً خَمْسَةَ عَشَرَ مِنْ قَوْمِ مُوسَی عَلَیْهِ السَّلاَمُ اَلَّذِینَ کَانُوا یَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ یَعْدِلُونَ وَسَبْعَةٌ مِنْ أَهْلِ اَلْکَهْفِ وَیُوشَعُ بْنُ نُونٍ وَ سَلْمَانُ وَ أَبُو دُجَانَةَ اَلْأَنْصَارِیُّ وَ اَلْمِقْدَادُ وَمَالِکٌ اَلْأَشْتَرُ فَیَکُونُونَ بَیْنَ یَدَیْهِ أَنْصَاراً أَوْ حُکَّاماً."

Qā’im (as) atatokea kutoka nyuma ya Ka‘bah akiwa na watu ishirini na saba: kumi na tano kutoka kwa kaumu ya Mūsā (as), waliokuwa wakiwalingania watu kwa haki na kwa hiyo wakihukumu, na saba kutoka kwa Ashāb al-Kahf, na Yūsha‘ bin Nūn, na Salmān, na Abū Dujānah al-Anṣārī, na Miqdād, na Mālik al-Ashtar. Hawa watakuwa pamoja naye kama wasaidizi au mahakimu. (Rawdhat al-Wā‘iẓīn, juzuu ya 2, uk. 266)

Utafiti huu unaendelea…

Imenukuliwa kutoka katika kitabu “Negin-e Āfarinish” huku ikifanyiwa marekebisho kiasi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha