Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, siku ya Jumatano, mashtaka hayo yaliwasilishwa kwa niaba ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Texas katika mahakama ya jiji la San Antonio, Marekani, na muungano wa kupinga ubaguzi nchini humo.
Katika kesi hiyo, rais wa Chuo Kikuu cha Texas, gavana wa jimbo hilo na maafisa wa utekelezaji wa sheria, wametuhumiwa kwa makusudi kukandamiza maandamano ya wanafunzi yaliyokuwa yakionyesha mshikamano na watu wanaodhulumiwa wa Palestina.
Kwa mujibu wa waraka wa kesi hiyo, rais wa chuo kwa kushirikiana na gavana "Greg Abbott" na polisi wa jimbo hilo, waliwapa maafisa vifaa vya kukabiliana na maandamano ili kuwavamia wanafunzi waliokuwa wakifanya maandamano ya amani jambo linalochukuliwa kuwa ni ukiukaji wa haki yao ya kutoa maoni kwa njia ya amani.
Mashtaka hayo yamechochea wimbi jipya miongoni mwa wanafunzi, na kuvuta uangalizi mkubwa zaidi kwa kesi za kisheria dhidi ya ubaguzi na ukiukwaji wa haki za wanafunzi katika vyuo vikuu vya Marekani.
"Arwin Hillerain", mwanafunzi wa mwaka wa pili, alisema katika mahojiano yake: “Katika kesi hii tunadai haki yetu, kwa sababu maafisa wanatuchukulia kana kwamba sisi ni waasi au wahalifu.”
Hillerain aliongeza kwa kusema: “Nililazimika kuacha somo langu la mafunzo bungeni (katika Bunge la Jimbo), na tangu nilipokamatwa nimepata matatizo ya afya ya akili.”
Cisco, mwanafunzi wa mwaka wa tatu, ambaye pia alikamatwa kutokana na kushiriki maandamano hayo, alisema: “Kesi hii ni muhimu sana, na imezua mijadala mingi kuhusu sera za upendeleo ambazo zinatekelezwa na serikali ya Trump.”
Makumi ya waandamanaji walikamatwa wakati wa maandamano huku wakifanyiwa ukatili mkubwa, lakini baada ya siku mbili, mwendesha mashtaka wa wilaya ya Travis aliwaachilia kwa kuwa hakukuwa na mashitaka yoyote dhidi yao.
Hata hivyo, kwa mujibu wa hati ya mashtaka, wanafunzi wote waliokamatwa, licha ya kuondolewa mashitaka, bado waliwekwa chini ya uangalizi wa kinidhamu na uongozi wa chuo.
Maoni yako