Alhamisi 1 Mei 2025 - 07:52
Baba wa kimaanawi (mlezi wa kiroho) wa Marjaa wa zama hizi wa Kishia

Miongoni mwa waliopata kunufaika moja kwa moja na masomo ya Haaj Sheikh, huko Qum au Arak, ni watu kama "Mirza Hashem Amoli, Muhammad Ali Araki, Sayyid Ahmad Husayni Zanjani, Sayyid Muhammad Damad, Sayyid Ahmad Khonsari, Sayyid Muhammad Taqi Khonsari, Sayyid Kazim Shari‘atmadari, Sayyid Muhammad Rida Gulpaayigani, Sayyid Shahabuddin Mar‘ashi Najafi, Sayyid Ruhullah Khomeini na Sayyid Sadruddin Sadr".

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, marehemu Ayatollah Ha’iri Yazdi, kwa kuasisi Hawza ya Qum, aliweka msingi wa mtaala wa kielimu ambao nyota angavu kama Imam Khomeini na Ayatollah Gulpaigani waliibuka kutoka humo.

Kwa kuwa "Ayatollah Sheikh Abdulkarim Ha’iri" alihusika kwa kiwango kikubwa angalau katika uanzishaji na uhuishaji wa taasisi mbili za kielimu huko Arak na Qum, kizazi cha wanazuoni wa Kishia kitaendelea kutoa huduma zake za kielimu na kiutendaji milele.

Miongoni mwa waliopata kunufaika moja kwa moja na masomo ya Haj Sheikh, huko Qum au Arak, ni watu kama Mirza Hashem Amoli, Muhammad Ali Araki, Sayyid Ahmad Husayni Zanjani, Sayyid Muhammad Damad, Sayyid Ahmad Khonsari, Sayyid Muhammad Taqi Khonsari, Sayyid Kazim Shari‘atmadari, Sayyid Muhammad Rida Gulpaigani, Sayyid Shahabuddin Mar‘ashi Najafi, Sayyid Ruhullah Khomeini na Sayyid Sadruddin Sadr.

Kila mmoja kati ya waliotajwa ima alifikia kuwa miongoni mwa wakubwa kielimu na uchaji Mola, au alipata hadhi ya kuwa marjaa wa waislamu wa Kishia.

Sheikh Murtadha Ha’iri, mtoto wa marehemu Ha’iri pia, aliyekuwa amepata tajriba ya kielimu kwa miaka mingi akiwa na baba yake, katika kipindi cha uongozi wa Ayatollah Buruujirdi, aliteuliwa kuwa mwakilishi wake huko Washington kwa ajili ya kufanya tabligh.

Uanzishaji wa Hawza kusambaa kwa sifa zake ndani ya Iran na ulimwenguni, kulisababisha Sheikh Abdulkarim apate heshima kubwa nchini Iran, kiasi kwamba Rizā Shāh ambaye karibu wakati ule ule aliingia madarakani sambamba na kuwasili kwa Sheikh mjini Qum, alijikuta akimtegemea Sheikh ili kufanikisha malengo yake.

Kutegemea huku, japokuwa katika baadhi ya nyanja kuliwezesha kupatikana kwa idhini ya kidini juu ya miradi ya kimaendeleo yenye mwelekeo wa kimagharibi ya Rizāshāh, lakini:

Kwanza, kulitoa fursa kwa taasisi za kidini na marjaa kurejea nafasi zao katika jamii ya Kiirani baada ya mabadiliko ya katiba, na kupangilia kwa utulivu mustakabali wao.

Pili, kulisababisha Hawza na viongozi wake wa kidini waweze kukabiliana na siasa kwa kutumia njia laini na kuzuia upotovu na miradi ya kupinga dini ya Rizāshāh, au angalau kuzuia kasi yake.

Chanzo: Kitabu Tabaqāt A‘lāmul-Shia, Agha Buzurg Tehrani, 1430 H.Q.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha