Jumapili 4 Mei 2025 - 08:19
Madaktari wanaoiunga mkono Palestina: Mkate si Bomu! Waacheni watoto wale chakula!

Hawza/ Muungano wa “Madaktari uliopo dhidi ya mauaji ya Kimbari” siku ya Jumatano walitoa kauli ya kuunga mkono watu wanyonge wa Ghaza na wakatoa wito wa kuondolewa haraka kabisa vizuizi huko Ghaza.

 Shirika la Habari la Hawza,/ Jumuiya ya Madaktari dhidi ya mauaji ya kimbari imeitaka Israel kusitisha kuwazingira watu wa Ghaza. Walielezea hali ya Ghaza kuwa ni ya dharura sana na kwamba mahitaji ya chakula na maji ni ya haraka mno.

Kundi hili lilitangaza kuwa: “Israel lazima isitishe vizuizi; watu wa Ghaza wanakufa kwa njaa na kiu. Zaidi ya watoto milioni moja ambao ni wagonjwa, majeruhi na wenye njaa, wapo katika hali mbaya kabisa na wanapoteza maisha yao huko Ghaza.”

Jeshi la utawala wa Kizayuni lilianza tena mashambulizi yake dhidi ya Ghaza tarehe 18 Machi, kwa kufanya ukatili mkubwa, baada ya kipindi kifupi cha kusitisha mashambulizi.

Madaktari wanachama wa kundi hili, huku wakiwa na mikate mikononi mwao, walipaza sauti katika jengo la Hart kama njia ya kuonesha kupinga kwao huku wakisema: “Mkate si bomu, waacheni watoto wale chakula.”

Karame Kummer, mtaalamu wa neva katika jiji la Boston, alisema: “Utapiamlo, njaa, na mashambulizi ya mfululizo dhidi ya watu wa Ghaza yanazidisha zaidi hitaji la huduma za afya.”

Daktari Brennan Bullman, ambaye hivi karibuni amerudi kutoka Ghaza, alisema: “Kwa kipindi cha wiki nane, hakuna msaada wala chakula kilichowasili Ghaza, na hali ni ya kutisha mno.”

Bullman aliongeza kwa kusena: “Kwa macho yangu mwenyewe niliona wauguzi na wenzangu waliopoteza jamaa zao huko Ghaza, wanalia kwa huzuni huku wanaendelea na kazi zao katika vituo vya afya.” Alitaka mapigano yaweze kusitishwa haraka iwezekanavyo.”

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa lilitangaza wiki iliyopita kuwa akiba yote ya chakula Ghaza imekwisha, na sasa watu wa Ghaza hawana hata mkate wa kula.

Watu milioni 2.4 wanaoishi Ghaza wamepoteza kila kitu kutokana na vita, na sasa wanategemea kabisa misaada ya kibinadamu, ambayo nayo imesitishwa tangu tarehe 2 Machi kwa sababu ya vizuizi vya Israel.

Zaidi ya Wapalestina 52,300 wameuawa katika mashambulizi ya kinyama ya Israel huko Ghaza tangia Oktoba 2023, ambapo wengi wao ni wanawake na watoto.

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai mnamo mwezi Novemba uliopita ilitoa hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wake wa zamani wa Ulinzi Yoav Gallant, kwa tuhuma za jinai za kivita na jinai dhidi ya ubinadamu huko Ghaza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha