Jumapili 4 Mei 2025 - 08:17
Nafasi ya vyombo vya habari katika kuonesha uhalifu unao fanywa na Israel ni ya kupongezwa

Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Raisi wa Baraza la Maulamaa wa kishia nchini Pakistan, katika ujumbe wake ulioandikwa kwa ajili ya kuadhimisha siku ya mnasaba wa Kimataifa ya uhuru wa vyombo vya Habari, amevitaja vyombo vya habari kuwa ni watumishi wa haki na ubinadamu, na amesifu juhudi za wanahabari katika kuonesha ukweli, hasa kuhusiana na jinai zinazo fanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wapalestina, kuwa ni za kupongezwa na zisizosahaulika.

Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya  Shirika la Habari la Hawza, Sayyid Sajid Ali Naqvi, katika ujumbe wake huo, akiwa Raisi wa Baraza la Maulamaa wa Kishia nchini Pakistan, amesisitiza juu ya nafasi ya juu ya vyombo vya habari katika kuhudumia haki na ubinadamu, na amebainisha kuwa uhuru wa vyombo vya habari ni miongoni mwa haki za msingi katika jamii, huku akilitaja jukumu la wanahabari katika kufichua dhulma hasa ile inayofanywa dhidi ya wapalestina na ukanda wa Ghaza kuwa ni la kupongezwa na la kudumu.

Katika ujumbe huo imetajwa kuwa: “Vyombo vya habari na uandishi wa habari ni jukumu zito na lenye umuhimu mkubwa, ambalo lengo lake ni kuongoza jamii, kufikisha ukweli na taarifa sahihi kwa watu bila upendeleo, ubaguzi au ushabiki wa wowote.”

Akiendelea na ujumbe wake, ameeleza kuwa vyombo vya habari vina nafasi ya kipekee katika ulimwengu wa leo, na kwamba duniani kote uhuru wa vyombo vya habari umeambatana na kujitolea kwa kiwango kikubwa na hata kufa kishahidi kwa baadhi ya wanahabari. Amesema kuwa kuadhimisha siku hii duniani ni kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari, na kutafuta njia ya kuondoa vizingiti na changamoto zinazowakabili waandishi wa habari.

Hujjatul-Islam Sajid Naqvi, akiwa anawakumbuka kwa heshima wanahabari waliouawa kishahidi hasa wale waliokuwa Palestina na Ghaza amesema: “Katika mazingira ya ukatili na unyama usio na kifani, walikuwa ni wanahabari walioonesha ujasiri wa hali ya juu na wakaonsha picha halisi ya dhulma dhidi ya watu wa Ghaza mbele ya macho ya dunia. Kujitolea kwao kutabakia milele katika kumbukumbu ya historia.”

Ameongeza kuwa: “Uhuru wa vyombo vya habari ni miongoni mwa haki za msingi za binadamu ambazo hazipaswi kuzuiwa. Ni wajibu wetu kuweka mazingira yatakayowawezesha wanahabari kutekeleza majukumu yao kwa uhuru na usalama. Katika dunia ya leo, nafasi ya vyombo vya habari vya kuchapisha na vya kielektroniki ni kubwa mno kiasi kwamba haiwezi kupuuzwa.”

Katika hitimisho la ujumbe huo, amesisitiza kuwa: “Vyombo vya habari vinapaswa kutumia nguvu zao zote katika kueneza maadili ya kiutu, kwani kutekeleza jukumu hili ni sawa na kutoka huduma muhimu ya kibinadamu na ni chombo chenye athari kubwa katika kuyapa maisha ya mwanadamu maana na mwelekeo sahihi.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha