Shirika la Habari la Hawza- Waziri Mkuu wa Malaysia, Mheshimiwa Datuk Seri Anwar Ibrahim, katika ufunguzi wa mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu nchini humo, alisema: Uelewa na umilikiji wa Qur'ani ndio msingi wa utukufu na maendeleo ya waislamu katika mataifa yao.
Aidha aliongeza kwa kusema: Bila shaka, katika dunia ya leo, umiliki wa lugha hai na zenye matumizi ya kila siku, pamoja na akili mnemba (AI), ni jambo lenye umuhimu mkubwa sana. Waislamu kamwe hawapaswi kubaki nyuma katika teknolojia hii ya kisasa. Kuachwa nyuma katika akili mnemba ni sawa na kuachwa nyuma kiuchumi na kiustaarabu.
Mheshimiwa Anwar Ibrahim aliendelea kusema: “Nawaomba marafiki zangu wenye elimu hii; nawaomba waislamu wengine wafafanue maarifa haya ndani ya jamii ya kiislamu kwa njia ya mipango ya makusudi, kwani sisi waislamu tunakabiliwa na changamoto zaidi, na suluhisho la changamoto hizi linahitaji tuwe wenye uhai zaidi na jasiri kuliko wakati wowote uliopita.”
Maoni yako