Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah A'raafi, Mudiri (Mkurugenzi) wa Hawzah Iran, alitoa rambirambi zake kufuatia kifo cha Papa Francis, kiongozi wa kanisa katoliki duniani. Maandishi ya ujumbe wake ni kama ifuatavyo:
بسم الله الرحمن الرحيم
Viongozi waheshimiwa wa Vatikani, na jamii ya Wakatoliki duniani,
Kwa salamu na heshima;
Kwa huzuni na masikitiko, tumepokea taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Papa Francis, kiongozi wa watu wa Kanisa Katoliki. Tunatoa rambirambi zetu kwa viongozi waheshimiwa wa Vatikani na kwa wafuasi wote wa dini ya kikristo kutokana na msiba huu mkubwa.
Papa Francis alikuwa mtu mashuhuri na mwenye ushawishi katika uwanja wa mazungumzo baina ya dini na katika kukuza amani na kuishi kwa maelewano baina ya mataifa. Yeye, kwenye mtazamo wa kibinadamu na kimaadili, alikuwa na juhudi zenye thamani katika kuimarisha uhusiano kwenye dini za mbinguni, hasa Uislamu na Ukristo, na katika kueneza maadili ya kiroho na kimaanawi, na kuhimiza uadilifu na kukataa dhuluma na uonevu duniani.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu aipumzishe roho yake, na tunaiombea jamii ya Wakatoliki subira na ustahamilivu.
Kwa kuendeleza heshima na kutoa rambirambi kwa mara nyingine tena,
Alireza A'raafi
Mkurugenzi wa Hawzah Iran
Maoni yako