Shirika la Habari la Hawza - Wananchi katika maandamano hayo walisisitiza kwamba suala la Palestina siyo tu suala la kisiasa, bali ni wito wa dhamira na utu, walisisitiza kuwa ili kumaliza mauaji ya halaiki, jamii zote za kimataifa zinapaswa kujitolea kwa dhati, walitaka kumalizika haraka kwa vizuizi dhidi ya Ghaza na mashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza.
Waandamanaji hao walikuwa wakitoa kaulimbiu kama isemayo "Tunaiunga mkono Ghaza, sitisheni mabomu dhidi ya Ghaza na Palestina huru," huku wakilaani vitendo vinavyo fanywa na utawala wa Kizayuni.
Vilevile, walikemea msaada wa Marekani usio na kikomo kwa Israel, huku wakiuita msaada huo kuwa wa kipumbavu na ndio chanzo kikuu cha ukatili unaoendelea kufanywa na Israel dhidi ya Ghaza.
Waandaji wa maandamano hayo waliiomba serikali ya Indonesia kuharakisha juhudi zake za kidiplomasia katika nyanja za kimataifa na kuleta haki kwa watu wa Ghaza.
Maoni yako