Alhamisi 18 Juni 2026 - 10:18
Maadili katika Ukusanyaji na Ulipaji wa Kodi Ni Msingi wa Maendeleo na Umoja wa Taifa

Hawza/ Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Maulana Sheikh Hemed Jalala, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili katika ukusanyaji na ulipaji wa kodi kwa akieleza kuwa; jambo hilo ni miongoni mwa nguzo muhimu zinazochangia maendeleo ya taifa, mshikamano wa kijamii na kuimarisha umoja wa kitaifa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Jalala alitoa kauli hiyo wakati akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na viongozi wa dini, lililolenga kujadili nafasi ya maadili katika mchakato wa ukusanyaji wa kodi na mchango wake katika ustawi wa nchi.

Akihutubia washiriki wa kongamano hilo, Sheikh Jalala alisema kuwa; kodi ni moja ya nyenzo muhimu zinazowezesha serikali kutoa huduma za msingi kwa wananchi, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kutimiza jukumu lake la kulipa kodi kwa uaminifu na uwajibikaji.

Aliongeza kuwa; maadili mema katika ukusanyaji na ulipaji wa kodi hujenga mazingira ya kuaminiana kati ya wananchi na taasisi za serikali, jambo ambalo huimarisha mshikamano wa kitaifa na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayowanufaisha wananchi wote.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, maafisa wa serikali na wadau wengine, ambapo washiriki walipata fursa ya kujadili umuhimu wa kuendeleza utamaduni wa uwajibikaji, uadilifu na ushirikiano katika masuala ya kodi.

Hafla hiyo ilifunguliwa rasmi na Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mcha Hassan Mcha, ambaye alieleza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za serikali na viongozi wa dini katika kuihamasisha jamii kuhusu wajibu wa kulipa kodi na kuzingatia maadili katika shughuli za kiuchumi.

Washiriki wa kongamano hilo walikubaliana kuwa; kuimarisha maadili katika mfumo wa kodi ni hatua muhimu katika kulijenga taifa lenye maendeleo endelevu, amani, mshikamano na ustawi wa wananchi wake.

Maadili katika Ukusanyaji na Ulipaji wa Kodi Ni Msingi wa Maendeleo na Umoja wa Taifa

Maadili katika Ukusanyaji na Ulipaji wa Kodi Ni Msingi wa Maendeleo na Umoja wa Taifa

Maadili katika Ukusanyaji na Ulipaji wa Kodi Ni Msingi wa Maendeleo na Umoja wa Taifa

Maadili katika Ukusanyaji na Ulipaji wa Kodi Ni Msingi wa Maendeleo na Umoja wa Taifa

Maadili katika Ukusanyaji na Ulipaji wa Kodi Ni Msingi wa Maendeleo na Umoja wa Taifa

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha