Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Muhammad Yazbak, Mkuu wa Baraza la Kisheria la Hizbullah, ametuma ujumbe kwa watu wavumilivu na wapiganaji mashujaa wa Lebanon.
Matini ya ujumbe ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote, Mlinzi wa Waumini na Mwangamizaji wa madhalimu. Rehema na amani zimshukie Mtume mtukufu na mkuu, Muhammad Mustafa, pamoja na Ahlul-Bayt wake watoharifu (as), hasa Hadhrat Baqiyyatullah, Hujjat bin Hasan Al-Mahdi (aj).
Enyi watu wetu na familia yetu, wahamiaji, wavumilivu na mlioshikamana nasi...
Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu; nyinyi ndio watoharifu zaidi, wenye ikhlasi zaidi, watukufu zaidi, wenye heshima zaidi na wenye utu zaidi. Nyinyi mpo chini ya kivuli cha rehema na fadhila za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ameteremsha utulivu katika nyoyo zenu pale aliposema:
(فَأَنزَلَ اللَّهُ سَکِینَتَهُ عَلَیٰ رَسُولِهِ وَعَلَی الْمُؤْمِنِینَ وَأَلْزَمَهُمْ کَلِمَةَ التَّقْوَیٰ)
"Basi Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume Wake na juu ya Waumini, na akawalazimisha kushikamana na neno la uchamungu.
" (Al-Fath: 6)
Na akaimarisha nyoyo zenu:
(وَلِیَرْبِطَ عَلَیٰ قُلُوبِکُمْ)
"Na ili azitie nguvu nyoyo zenu.
" (Al-Anfal: 11)
Subira yenu, kutarajia malipo ya Mwenyezi Mungu na ustahimilivu wenu vinatokana na uoni na nuru ya nyoyo zenu, huu ni uaminifu wenu wa kweli kwa mpendwa wa haki yenu; kwa vile mliikataa batili, udhalili na fedheha, nyinyi ni watu wa heshima:
(وَلِلَّهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِینَ)
"Na heshima ni ya Mwenyezi Mungu, ya Mtume Wake na ya Waumini."
(Al-Munafiqun: 8)
Tuko pamoja nanyi katika maumivu na taabu, na kwa pamoja, Inshaallah, tuna fursa ya ushindi siku za usoni:
(مَتَیٰ نَصْرُ اللَّهِ ۗ أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّهِ قَرِیبٌ)
"...Msaada wa Mwenyezi Mungu utakuja lini? Jueni kwamba msaada wa Mwenyezi Mungu upo karibu."
(Al-Baqarah: 214)
Sisi tuko juu ya ahadi ya shahidi wetu mtukufu na mtakatifu ambaye alitupa bishara ya ushindi kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu:
(إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِینَ آمَنُوا فِی الْحَیَاةِ الدُّنْیَا وَیَوْمَ یَقُومُ الْأَشْهَادُ)
"Hakika tutawanusuru Mitume wetu na wale walioamini katika maisha ya dunia na siku watakaposimama mashahidi.
" (Ghafir: 51)
Enyi wapiganaji mashujaa...
Amani iwe juu ya wapenzi ambao kwa nafsi zilizounganishwa na heshima ya Mwenyezi Mungu na Al-Quds, kwa irada, azma na yakini juu ya kauli ya Mwenyezi Mungu:
(إِن یَنصُرْکُمُ اللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَکُمْ)
"Ikiwa Mwenyezi Mungu atakusaidieni, basi hakuna yeyote atakayewashinda."
(Aali Imran: 160)
Haikufai nyinyi isipokuwa yale ambayo Amirul-Muuminina Ali (as) alisema kuhusu masahaba wa Mtume Mtukufu (saww):
"Nimewaona masahaba wa Muhammad (saww), lakini sioni yeyote miongoni mwenu anayefanana nao, Walikuwa wanaamka asubuhi wakiwa wamevurugika nywele na wamejaa vumbi, huku wakiwa wamepitisha usiku wao kwenye kusujudu na kusimama kwa ibada, wakati mwingine walikuwa wakiweka mapaji vya nyuso zao ardhini mbele ya Mwenyezi Mungu, Kwa kuikumbuka Akhera walikuwa kana kwamba wanasimama juu ya makaa ya moto, wenye wasiwasi na mtetemeko, kutokana na kusujudu kwa muda mrefu, mapaji yao yalikuwa na alama kama magoti ya mbuzi, Mwenyezi Mungu alipotajwa macho yao yalitiririka machozi kiasi cha kulowesha nguo zao, na walitetemeka kama miti inavyotikisika siku yenye upepo mkali, kwa hofu ya adhabu na matumaini ya thawabu.”
Nyinyi hasa ni miongoni mwa Mawalii wa Mwenyezi Mungu, kama Amirul-Muuminina (as) alivyosema:
"Ama baada ya hayo, hakika jihadi ni mlango miongoni mwa milango ya Pepo ambao Mwenyezi Mungu ameufungua kwa ajili ya Mawalii wake maalumu, nayo ni vazi la uchamungu, ngao imara ya Mwenyezi Mungu na kinga yake madhubuti."
Enyi Mujahidina mashujaa! Mwenyezi Mungu atawaadhibu maadui zenu kupitia mikono yenu na kwa kujitolea kwenu atawadhalilisha viongozi wao na wale wanaofanya uchochezi na upotoshaji kupitia vyombo vya habari.
(قَاتِلُوهُمْ یُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَیْدِیکُمْ وَیُخْزِهِمْ وَیَنصُرْکُمْ عَلَیْهِمْ وَیَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِینَ وَیُذْهِبْ غَیْظَ قُلُوبِهِمْ)
"Pigana nao; Mwenyezi Mungu atawaadhibu kupitia mikono yenu, atawadhalilisha, atawapa ushindi dhidi yao na ataponya nyoyo za Waumini na kuondoa hasira zilizomo ndani ya nyoyo zao." (Tawbah: 14–15)
Enyi watu wa Hussein, enyi wajenzi wa taifa na walinzi wa mamlaka yake na watu wake, watu wenye heshima na walio huru wapo pamoja nanyi, damu zenu safi zinajenga, na damu inayotoka kwenye majeraha yenu ni damu ya majeraha ya taifa; haitapona isipokuwa kwa kuisafisha ardhi yake kutokana na uchafu wa Kizayuni na Marekani.
Amani iwe juu ya wale ambao Mwenyezi Mungu amewafanya kuwa mashahidi:
(وَیَتَّخِذَ مِنکُمْ شُهَدَاءَ)
"Na Mwenyezi Mungu awafanye baadhi yenu kuwa mashahidi."
(Aali Imran: 140)
Na juu ya majeruhi mashahidi walio hai, juu ya mateka walio huru, na juu ya familia zenu safi ambapo mmekuwa wa mbele katika kutoa na thabiti zaidi katika misimamo.
Hatutaachana na msimamo wetu, hata kama utasababisha makabiliano ya Hussein
Enyi wapendwa wenye heshima...
Tulivumilia kwa miezi mingi baada ya makubaliano kati ya serikali na adui, kwa kutarajia malipo ya Mwenyezi Mungu. Serikali ilibeba jukumu la kulinda wananchi wake, mamlaka yake na kumfuatilia adui ili kutekeleza masharti ya makubaliano.
Sisi tulijifunga nayo, tukayatekeleza na tukatoa mamia ya mashahidi pamoja na zaidi ya majeruhi elfu moja kutokana na mashambulizi ya adui, pamoja na uharibifu, maangamizi na kupenya kwa adui katika maeneo ambayo kabla ya makubaliano hakuweza kuyafikia.
Tuliipa serikali nafasi hadi pale tuliposhindwa kuvumilia tena, tulichukua fursa mwafaka baada ya kauli za mara kwa mara kwamba subira yetu ina mipaka katika kumjibu adui mshenzi.
Mamlaka zilizopo zilichochewa na kuchukua uamuzi wao mbaya, na zakawa zinamtumikia adui wa Kizayuni na Marekani, iwe kwa kujua au kutokujua, kwamba wapinzani wako nje ya uhalali wa kisheria.
Wakati huo adui alisema: "Hatuna tatizo na Lebanon; tatizo letu ni Hizbullah ya kigaidi."
Kama ambavyo baadhi katika Baraza la Mawaziri walijaribu kuuita Muqawama kuwa ni ugaidi.
Serikali iliingia katika mazungumzo ya moja kwa moja na adui pamoja na upatanishi wa Marekani, ambaye ni mshirika wa adui katika vita vyake.
Kwa hiyo sisi pamoja na watu wetu wavumilivu tulisema: "Yale yanayopita Washington ya kujisalimisha hayana umuhimu wowote kwetu."
Basi kila mtu asikie; matakwa yetu ambayo damu, kujitolea na mateso yalitolewa kwa ajili yake ni haya:
Kwanza: Kusitishwa kwa vita kikamilifu na kusimamishwa kwa mashambulizi ya ardhini, baharini na angani.
Pili: Kuondoka kikamilifu kutoka ardhi ya taifa.
Tatu: Kurejea wananchi katika miji na vijiji vyao hadi mipakani.
Nne: Kujenga upya maeneo hayo yawe mazuri zaidi kuliko hapo awali, hata vijiji vya mpakani.
Tano: Kuachiliwa na kupewa uhuru mateka.
Sita: Tuelekee katika utekelezaji wa kauli ya Rais kuhusu mazungumzo ya mkakati wa ulinzi au usalama wa taifa.
Huu ndio msimamo wetu; hatutaachana nao, hata kama utasababisha makabiliano ya Hussein na kufikia moja ya mema mawili — shahada au ushindi.
Enyi watu wetu na enyi wapiganaji mashujaa, sisi ni waaminifu kwa ahadi yetu kwenu.
Tunawashukuru wote wanaotunyoshea mkono wa msaada na utetezi, na kwa namna ya pekee tunaishukuru Jamhuri ya Kiislamu na Kiongozi wake mtukufu, Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, pamoja na viongozi wote walio na wasiwasi juu yetu; wale wanaotekeleza jukumu lao katika mazungumzo na kuleta usitishaji wa vita kikamilifu kwa Lebanon na nyanja za Muqawama.
Enyi watu wetu, furahini! Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, tuko karibu na ukombozi wa tatu.
Na amani iwe juu yenu.
Maoni yako