Ijumaa 3 Aprili 2026 - 00:45
Pandeni mche wa matumaini katika upeo wa Iran / Kila hatua katika mwelekeo wa kupanua ustawi na kujenga mustakabali angavu wa Iran ni kitendo stahili na kinachofaa

Hawza/ Wakati huu ambapo adui mdhalimu na asiye na huruma wa Kimarekani na Kizayuni hana mipaka ya kibinadamu, na kimaadili katika unyama wake, na hata maeneo ya asili na mazingira ya nchi yetu pendwa ameingilia kuyashambulia na kuyadhuru, basi kila hatua katika njia ya kukuza ustawi na kujenga mustakabali angavu wa Iran ni kitendo stahiki na kinachofaa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, maandishi ya ujumbe wa Mtukufu Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika mnasaba wa kuadhimisha Siku ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Siku ya Asili, ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Yeye ndiye aliye kuumbeni katika ardhi, na akakuwekeni humo.

Taifa jasiri la Iran mwaka huu wa Nouruz limeuchanganya msimu huu na ujasiri na hamasa, na baada ya kuadhimisha tarehe 12 Farvardin (1 April 2026) — Siku ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran — wanaelekea kuipokea Siku ya Asili.

Wakati huu ambapo adui mdhalimu na asiye na huruma wa Kimarekani na Kizayuni hana mipaka ya kibinadamu na kimaadili katika unyama wake, na hata maeneo ya asili na mazingira ya nchi yetu pendwa ameingilia kuyashambulia na kuyadhuru, basi kila hatua katika njia ya kukuza ustawi na kujenga mustakabali angavu wa Iran ni kitendo stahiki na kinachofaa.

Miongoni mwa matendo haya yanayopendeza ni kwamba; watu wote mijini na vijijini, kwa kusaidiana na kwa ushirikiano na uratibu wa taasisi husika, kuanzia Siku ya Asili hadi mwisho wa majira ya kuchipua — hasa siku za mwezi wa Farvardin — wachukue hatua ya kupanda miti yenye matunda pamoja na kutekeleza uangalizi na matunzo yanayohitajika baadaye.

Marekani na Mzayuni mwenye tabia za kishetani wanaoua watoto, waliwaua kinyama chipukizi wa shule ya Shajarat Tayyiba; lakini taifa la Iran, kwa nia ya mashahidi wote, hasa mashahidi wa Vita vya Kulazimishwa vya Tatu, linalipandikiza mche wa matumaini katika eneo lote la nchi yake ili kila mche kati ya hii, katika miaka ijayo, ubadilike kuwa mti mwema na wenye matunda tele, Inshaallah.

Sayyid Mojtaba Hosseini Khamenei

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha