Jumatatu 6 Oktoba 2025 - 22:15
Wataliano wataka mechi kati yao dhidi ya Israel Ifutwe

Hawza/ waandamanaji siku ya Ijumaa waliingia kwenye mazoezi ya timu ya taifa ya kandanda ya Italia, na baada ya kukaribia lango na uwanja, walitangaza kuwa wanataka mchezo wa timu yao dhidi ya Israel ufutwe, kutokana na mauaji ya kimbari yanayoendelea huko Ghaza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, maandamano haya makubwa yalifanyika sambamba na mgomo wa kitaifa nchini Italia ulioitishwa ili kulaani mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza. Italia imepangwa kuwa mwenyeji wa timu ya Israel tarehe 14 Oktoba katika mji wa Udine. Hata hivyo, UEFA, kwa mujibu wa ombi la wanachama wengi, imeweka kwenye ajenda yake kusimamishwa kwa timu ya Israel.

Waandamanaji wa Kiitaliano walikusanyika kwa utulivu na bila vurugu kwenye uwanja wa mpira, wakitoa kauli mbiu kama:

“Acheni tuuzuie Uzayuni kwa njia ya Muqawama .” “Mnawezaje kucheza mpira na Israel ambayo ni nchi ya kihalifu?”

Aidha, siku ya Ijumaa pia wafanyakazi na wanafunzi wengi walifanya maandamano katika nchi mbalimbali kulaani kukamatwa na kufukuzwa kwa wanachama wa meli zilizobeba misaada ya kibinadamu kuelekea Ghaza.

Chanzo: Al Jazeera

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha