Alhamisi 11 Septemba 2025 - 14:27
Nafasi ya (Intidhar) Kusubiria faraja katika Utamaduni wa Kishia (Sehemu ya Pili)

Hawza / Katika maana hii, mafundisho ya dini yamekusudia, mbali na kubainisha fadhila ya “faraja ya kijamii” na matumaini ya siku zijazo na kuelekeza wanadamu kwenye uwanja huu, kulaani pia kukata tamaa.

Shirika la Habari la Hawza: Katika uchunguzi mfupi, riwaya zinazozungumzia kuhusiana na kusubiri zimegawanywa katika makundi makuu mawili:

Kungojea faraja kwa maana ya kijumla

Katika maana hii, mafundisho ya dini yamekusudia, mbali na kubainisha fadhila ya “faraja ya kijamii” na matumaini ya siku zijazo na kuelekeza wanadamu kwenye uwanja huu, kulaani pia kukata tamaa.

Umuhimu wa mafundisho ya Kiislamu katika kubainisha maana ya kijumla ya kungojea na matumaini ni wa kiwango ambacho umekutaja kwa majina ya juu zaidi na kutaja thamani za ajabu kwa ajili yake, Blbaadhi ya majina hayo ni kama yafuatayo:

Ibada na Utumishi

Qur’an na Ahlulbayt (a.s) hutufundisha kwamba lengo la uumbaji ni kumwabudu Mwenyezi Mungu.

(Adh-Dhariyat (51): Aya ya 56)

Mtume Mtukufu wa Uislamu (s.a.w.w) amehesabu moja ya sura za ibada hii kuwa ni kungojea faraja na akasema:

«اِنتِظارُ الفَرَجِ عِبَادَةٌ»

Kungojea faraja ni ibada
(Shaykh Tusi, Al-Amali, uk. 405)

Kwa kuwa ibada nyingi zimo katika orodha ya matendo ya mwanadamu, inaweza kutolewa natija kwamba hapa pia makusudio ya kungojea ni mkusanyiko wa mienendo mahsusi.

Ibada iliyo bora zaidi

Baadhi ya ibada zina ubora juu ya nyingine; kwa hivyo kuzitekeleza, mbali na kusisitizwa na mafundisho ya dini, pia zina thawabu zaidi, na mchango wake katika kujenga utu wa mwanadamu huwa mkubwa zaidi.

Mtume Mtukufu wa Uislamu (s.a.w.w), baada ya kutazama dhana hii ya kungojea faraja kuwa ni miongoni mwa ibada za Mwenyezi Mungu, ameitaja pia kuwa moja ya ibada bora zaidi na akasema:

«اَفضَلُ العِبادَةِ اِنتِظارُ الفَرَجِ»

Ibada bora zaidi ni kungojea faraja
(Kamalud-Din wa Tamamun-Ni‘mah, j.1, uk. 287)

Kazi bora zaidi

Wakati mwingine, ameitambulisha pia kuwa ni kazi bora zaidi miongoni mwa umma wa Mtume wa Mwisho (s.a.w.w).

Mtume Mtukufu wa Uislamu (s.a.w.w) amesema:

«اَفْضَلُ اَعْمالِ اُمَّتِی اِنتظارُ الفَرَجِ مِنَ اللَّهِ عَزَّوَجَلَّ»

Kazi bora zaidi kwa umma wangu ni kungojea faraja kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu
(Kamalud-Din wa Tamamun-Ni‘mah, j.2, uk. 644)

Faraj yenyewe kuwa ni faraja

Leo hii, kwa mujibu wa elimu ya saikolojia, imebainishwa kwamba kuwa na matumaini kuna mchango mkubwa sana katika mienendo ya kijamii, kwa maneno mengine, kusubiri mustakabali ulio na nuru na mng’ao husababisha maisha ya sasa ya mwanadamu pia yakae na mwanga na uhai.

Katika baadhi ya riwaya zinazohusiana na kungojea faraja, ukweli huu wenye thamani umetajwa kwa namna hii kwamba kungojea faraja, yenyewe ni aina ya faraja na ufungukaji.

Imam Sajjad (a.s) amesema:

«اِنتِظارُ الفَرَجِ مِنْ اَعظَمِ الفَرَجِ»

Kungoja faraja ni miongoni mwa faraja mkubwa zaidi
(Kamalud-Din wa Tamamun-Ni‘mah, j.1, uk. 319)

Jihadi bora zaidi

Katika mafundisho ya dini, jihadi na jitihada katika njia ya Mwenyezi Mungu imehesabiwa kuwa ni moja ya mienendo muhimu sana ya mtu binafsi na ya kijamii ya Waislamu. Aya nyingi za Qur’an na riwaya nyingi kutoka kwa Maimamu watoharifu (a.s) zimeashiria ukweli wa tendo hili lenye thamani.

Kuhusu umuhimu wa kungojea faraja, mbali na yale yaliyotajwa, tunakutana na riwaya ambazo ni za kushangaza sana, nazo ni kwamba kungojea kumehesabiwa si tu kama “jihadi” bali “jihadi bora zaidi.” Kutoka kwenye riwaya hizi inapatikana wazi kwamba kungojea ni miongoni mwa matendo.

Mtume Mtukufu wa Uislamu (s.a.w.w) amesema:

«اَفْضَلُ جِهادِ اُمَّتی اِنْتِظارُ الفَرَجِ»

Jihadi bora zaidi kwa umma wangu ni kungojea faraja
(Tuhaf al-‘Uqul, uk. 37)

Hukumu dhidi ya kukata tamaa

Kinyume na mafundisho haya ya juu, kukata tamaa na kuvunjika moyo kutokana na rehema za Mola Mlezi kumelaaniwa vikali na kuhesabiwa miongoni mwa madhambi makubwa.

(Surat Yusuf (12): Aya ya 87)

Utafiti huu unaendelea…

Imenukuliwa kutoka kwenye kitabu kiitwacho: Darsnameh Mahdawiyat, kilichoandikwa na Khodamorad Salimiyan, huku ikifanyiwa mabadiliko kiasi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha