Jumapili 3 Agosti 2025 - 15:48
Je, Kuona Picha za Njaa huko Ghaza Kunaathiri Fikra za watu nchini Israel?

Hawza/ Kwa mara ya kwanza tangia kuanza kwa vita vya sasa vya Ghaza, Kituo cha Televisheni cha Channel 12 cha utawala wa Kizayuni kimeonyesha video yenye picha na filamu za watoto waliokonda kwa njaa na familia zao zilizokata tamaa, wakati uchezaji wa picha hizi umeleta hisia za huruma na ukosoaji, wachambuzi wanasema kwa kuzingatia ufahamu wao wa jamii ya Israel, ni vigumu kuamini kwamba jambo hili litakuwa na athari kubwa kwa fikra za umma.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Channel 12 ya utawala wa Kizayuni kwa mara ya kwanza imeonyesha picha za kushtua za njaa na ukosefu wa chakula huko Ghaza, jambo lililofanya Waisraeli kuwa katika mstari wa mbele wa habari za dunia kuhusu usababishaji wa njaa na kuzuia misaada ya kibinadamu.

Baada ya kurushwa kwa picha hizo, na baada ya mtangazaji wa kipindi, Yonit Levi, kufikia hitimisho kwamba imewadia wakati wa kuziona picha hizi kama kushindwa kwa maadili kwa Israel na si kushindwa kwa vyombo vya habari, alikabiliwa na upinzani na ukosoaji mkali kutoka kwa watazamaji wengi, na baadhi ya watu wa Israel walitaka marufuku ya kurushwa kwa filamu za aina hiyo.

Kwa mujibu wa tafiti za maoni, Waisraeli wengi wanataka vita vikome na wafungwa wa vita wa Kizayuni waachiwe huru, takwimu hizi, ambazo zinatokana na tafiti, miongoni mwa Waarabu wa Israel zimefikia hata asilimia 89.

Hata hivyo, bado watu wengi wa Israel wanaamini kwamba picha za mateso ya Ghaza ni za kutengenezwa na hazina uhalisia. Wanaulaumu jeshi la Israel kwa udhaifu wa utendaji kuhusiana na kuachiwa kwa mateka wa Kizayuni, na wanazungumzia suala hili katika maandamano yao.

Chanzo: Siasa za Nje

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha