Ijumaa 25 Julai 2025 - 23:44
Ujumbe wa Kiongozi wa Mpinduzi kwa mnasaba wa maafhimisho ya siku ya kupata shahada kundi miongoni mwa wananchi wa Irani, makamanda wa kijeshi na wanasayansi wa nyuklia

Hawza/ Kwa mnasaba wa siku ya arubaini tangia kupata shahada kundi la wananchi, makamanda wa jeshi waliobobea na wanasayansi mashuhuri wa nyuklia wa nchi hii kwa mikono ya utawala muovu na mhalifu wa Kizayuni, Mtukufu Ayatollah Khamenei ametoa ujumbe.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Matni ya ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Bismillāhi ar-Raḥmāni ar-Raḥīm

Taifa tukufu la Iran!
Siku ya arubaini tangia kupata shahada kundi la wananchi wetu wapendwa imewadia, ambao miongoni mwao walikuwapo makamanda wa kijeshi waliobobea na wanasayansi mashuhuri wa nyuklia. Pigo hili limetolewa na kundi tawala la kizayuni lililojaa uovu na uhalifu, ambalo ni adui muaovu na wa kinafiki zaidi kwa taifa la Iran, bila shaka, kuondokewa na makamanda kama mashahidi Baqeri, Salami, Rashid, Hajizadeh, na Shadmani pamoja na wanajeshi wengine, na vilevile wanasayansi kama mashahidi Tehranchi, Abbasi na wanasayansi wengine, ni jambo zito kwa kila taifa, hata hivyo, adui mpumbavu na mwenye mtazamo mfupi hakufikia lengo lake, mustakabali utaonyesha kwamba harakati zote mbili—ya kijeshi na ya kielimu—zitaendelea kwa kasi zaidi kuliko ilivyokuwa zamani, kuelekea kwenye malengo makuu inshāAllāh.

Mashahidi wetu wenyewe walichagua njia ambayo ndani yake uwezekano wa kufikia daraja ya juu ya shahada haukuwa haba, na hatimaye wakafikia kile ambacho ni matumaini ya kila mwenye kujitoa mhanga; hongera kwao; lakini machungu ya jambo hilo kwa taifa la Iran, hasa kwa familia za mashahidi na hasa wale waliowajua kwa karibu, ni makubwa na mazito.

Katika tukio hili pia, kuna mambo yenye mwangaza yanayoonekana kwa uwazi:

Kwanza, uvumilivu, subira na uimara wa kiroho kwa waliobaki, jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa kwa namna hii isipokuwa ndani ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Pili, ustahimilivu na uthabiti wa taasisi zilizokuwa chini ya uongozi wa mashahidi hao, ambazo hazikuruhusu pigo hili kubwa kuondoa fursa na kuzuia mwendo wao.

Na tatu, adhama ya ustahimilivu wa kimiujiza wa taifa la Iran ambayo ilidhihirika katika umoja, uimara wa roho na azma madhubuti ya watu wake ya kusimama kwa pamoja katika uwanja wa mapambano, Iran ya Kiislamu katika tukio hili kwa mara nyingine imeonyesha uimara kwenye misingi yake.

Iran ya Kiislamu, kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu, kila siku itakuwa imara zaidi kwa idhini ya Allah.

Jambo muhimu ni kwamba tusighafilike na ukweli huu, wala wajibu unao tokana nao,
Kulinda umoja wa kitaifa ni jukumu la kila mmoja wetu, Kasi inayotakiwa katika maendeleo ya kielimu na kiteknolojia katika nyanja zote ni jukumu la wasomi., kulinda heshima na hadhi ya nchi na taifa ni wajibu usio na upendeleo kwa wasemaji na waandishi, Kuiandaa nchi kila siku zaidi kwa zana za kulinda usalama na uhuru wa kitaifa ni jukumu la makamanda wa kijeshi, kujitahidi kufuatilia na kufanikisha kazi za nchi ni wajibu wa taasisi zote za kiutendaji Kuongoza kiroho na kuangaza nyoyo na kuhimiza subira, utulivu na uthabiti wa watu ni jukumu la maulamaa, na kulinda hamasa, shauku na uelewa wa kimapinduzi ni wajibu wa kila mmoja wetu, hasa vijana.
Mwenyezi Mungu Mwenye Ukarimu na Rehema awape wote mafanikio.

Salamu kwa taifa la Iran, na salamu kwa vijana mashahidi, kwa wanawake na watoto mashahidi, na kwa mashahidi wote na wafiwa wao.

Wassalāmu ʿalaykum wa raḥmatullāh


Sayyid ‘Ali Khamenei
3 Mordad 1404 (Hijria Shamsiyya)

July 25, 2025

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha