Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, kutokana na mnasaba wa siku arobaini za mashahidi wa vita vya kulazimishwa vya siku 12 vilivyo anzishwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya taifa la Iran, leo hii hafla ya kumbukumbu ya mashahidi hao imeandaliwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Husainiya ya Imam Khomeni (r.a) huku ikuhudhuriwa na familia za mashahidi, makundi mbalimbali ya wananchi, na pia kwa uwepo wa kundi la viongozi.
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika hafla hii, katika hotuba zake, aliita vita hivi kuwa ni sababu ya kudhihiri kwa azma na nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu na kuonesha uimara usio na kifani wa misingi yake, na kwa kusisitiza kwamba chanzo kikuu cha uadui ni upinzani wa mahasidi dhidi ya imani, elimu, na mshikamano wa taifa la Iran, alisema kuwz: “Taifa letu, kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu, halitaacha njia ya kuimarisha imani na kueneza elimu mbalimbali, na kutokana na upofu wa adui tutaweza kuipeleka Iran kwenye kilele cha maendeleo na heshima.”
Mtukufu Ayatollah Khamenei, huku akitoa tena rambirambi kwa wafiwa wa makamanda wa kijeshi, wanasayansi, na wananchi wapendwa waliouawa shahidi katika vita vya hivi karibuni, alibainisha kuwa: “Taifa la Iran, pamoja na heshima kubwa ilizopata katika siku hizi 12 ambazo leo dunia nzima inazikiri, liliweza kuonesha nguvu, ustahimilivu, azma na dhamira, kiasi ch kwamba kila mtu alihisi kwa karibu nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu.”
Yeye alikutaja kudhihiri kwa uimara usio na kifani kwa misingi ya Jamhuri ya Kiislamu kuwa ni miongoni mwa sifa nyingine za vita hivi vya karibuni, na akaongeza: “Matukio haya hayakuwa ya kipekee kwetu, na Jamhuri ya Kiislamu katika kipindi cha miaka 46 iliyopita, mbali na vita vya kulazimishwa vya miaka minane, Iran mara kadhaa imekabiliana na matukio kama mapinduzi, fitina mbalimbali za kijeshi, kisiasa na kiusalama, na kushinikizwa kwa watu dhaifu kuchukua hatua dhidi ya taifa, na imezizima njama zote za adui.”
Kiongozi wa Mapinduzi aliuita msingi wa Jamhuri ya Kiislamu kuwa ni nguzo mbili za “dini” na “elimu”, na akasema: “Wananchi na vijana wa Iran kwa kutegemea nguzo hizi mbili, wamemlazimisha adui kurudi nyuma katika nyanja mbalimbali, na kuanzia sasa pia wataendelea kufanya hivyo.”
Yeye aliitaja sababu kuu ya upinzani wa ubeberu wa kimataifa na hasa Marekani dhalimu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kuwa ni dini na elimu na mshikamano wa Wairani chini ya kivuli cha Qur’ani na Uislamu, na akasema: “Kile wanachokitaja kuwa ni nyuklia, urutubishaji, na haki za binadamu ni visingizio, na sababu halisi ya huzuni na upinzani wao ni kuibuka kwa kauli mpya na uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu katika nyanja mbalimbali za kielimu na maarifa ya kibinadamu, kiteknolojia, na kidini.”
Mtukufu Ayatollah Khamenei, kwa kusisitiza kwamba taifa la Iran kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu halitaacha dini na elimu yake, aliongeza kwa kusema: “Sisi katika njia ya kuimarisha dini na kueneza na kuimarisha elimu mbalimbali tutachukua hatua kubwa, na kutokana na upofu wa adui tutaweza kuipeleka Iran kwenye kilele cha maendeleo na heshima.”
Maoni yako