Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, kufuatia kutoweka kwa Hujjatul-Islam Ghulam Hasnain Wajdani, Imamu wa Ijumaa wa mji wa Quetta, nchini Saudi Arabia, wananchi na wanazuoni wa mji huo kwa kufanya maandamano ya kupinga tukio hilo wametaka serikali ya Pakistan ichukue hatua za haraka na zenye ufanisi kwa ajili ya kuachiwa huru mwanazuoni huyo mashuhuri.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa kwa wingi na wanazuoni, wakubwa wa mji, vijana na familia mbalimbali, washiriki kwa kutoa kauli mbiu waliitaka serikali ichukue hatua madhubuti kuhusu hali ya mwanazuoni huyo wa dini ambaye hadi sasa kwa zaidi ya miezi mitatu yupo mikononi mwa maafisa wa Saudi Arabia bila ya kuwepo shtaka lolote rasmi dhidi yake.
Wananchi waliokuwa wakipinga tukio hilo waliitaka serikali ya Pakistan kutumia nyenzo zake za kidiplomasia na rasmi, kupeleka suala la kukamatwa kinyume na haki kwa Hujjatul-Islam Wajdani katika ngazi ya kimataifa na kwa njia ya mazungumzo na maafisa wa Saudi Arabia kufanya juhudi za haraka na zisizo na masharti kwa ajili ya kuachiwa kwake.
Kwa mujibu wa ripoti, Hujjatul-Islam Hasnain Wajdani alisafiri kuelekea Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija, lakini tangu kuingia kwake nchini humo hadi sasa hakuna taarifa yoyote ya uhakika kuhusu mahali anaposhikiliwa au hali yake ya afya, kutojulikana huku kwa muda mrefu kumezusha wasiwasi mkubwa kwa familia yake, wanafunzi wake na tabaka mbalimbali za jamii ya kidini ya Pakistan.
Hujjatul-Islam Ghulam Hasnain Wajdani ni miongoni mwa wanazuoni mashuhuri na wanaoheshimika wa Pakistan ambaye daima katika hotuba zake amesisitiza juu ya umoja wa Waislamu na alikuwa mstari wa mbele katika kueneza fikra ya karibu na mshikamano wa Kiislamu katika eneo hilo.
Wananchi na wanazuoni kwa kusisitiza hadhi ya kielimu, kimaadili na kijamii ya mwanazuoni huyu mwenye hekima, wameitaka serikali ya Pakistan kwa umakini na uwajibikaji ichukue hatua katika kutetea haki za raia wake, hususan watu wa dini, na kuzipa kipaumbele juhudi za kuachiwa huru kwa mwanazuoni huyu aliyedhulumiwa.
Maoni yako