Jumapili 3 Agosti 2025 - 15:52
UNICEF: Watoto wa Gaza wanapumua pumzi za mwisho

Hawza/ Shirika la Afya Duniani limewaomba watu dunianj kuchukua hatua za haraka kwa ajili ya Ghaza, kwani Ghaza kwa sasa ni mahali ambapo watoto wanakufa kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa kutokana na kuzingirwa na vita vya Israel!

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Bw. Ted Chaiban, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la UNICEF (Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa) alisema: Leo, lazima umakini wetu wote uwe juu ya Ghaza! Mateso ya Ghaza ndiyo tatizo kali na la dharura zaidi kwa sasa, na watoto wanakufa kwa kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa!

Chaiban, katika kikao kilichofanyika kuhusu ziara yake ya Mashariki ya Kati, aliongeza kwa kusema: Sasa tuko mahali ambapo tunapaswa kufanya maamuzi sahihi na ya kuamua hatima, mahali ambapo itaamuliwa kama watoto elfu kumi waliokosa chakula wataishi au la.

Akasema: Sote tunaona picha za watoto waliokosa chakula na tunajua nini kinaendelea, lakini mimi nilikuwa pale na nikaona kwa macho yangu; ni hali ya kuumiza sana na inayotikisa moyo!

Chaiban katika ziara yake ya hivi karibuni alitembelea Israel na pia Ghaza, na vilevile alienda Ukingo wa Magharibi, akibainisha kuwa, hii ni ziara yake ya nne katika maeneo haya tangu kuanza kwa vita vya utawala wa Kizayuni.

Alisisitiza kwamba tangu mwanzoni wa vita vya sasa, zaidi ya watoto 18,000 huko Ghaza wameuawa kishahidi.

Gaza inakabiliana na njaa kali

Kwa sasa Ghaza inakabiliana na hatari kubwa ya njaa; kati ya kila watu watatu, mmoja hana chakula wala maji! Viwango vya utapiamlo vimepita hata kiwango cha njaa, zaidi ya asilimia 16.5 ya watu hawana chochote cha kula na wako katika njaa ya kutisha! "Watu duniani, fanyeni jambo kwa ajili ya Ghaza!

Katika kujibu swali la mwandishi mmoja kuhusu misaada ya angani, Chaiban aliongeza: Angalieni, hali ya Ghaza ni ya dharura kiasi kwamba ni lazima kutumia kila mbinu ya kutoa msaada, lakini misaada ya angani haiwezi kamwe kufikia kiwango cha usafirishaji wa misaada kwa malori na meli, na kwa hakika haitoshi.

Chanzo: Shirika la Habari la Anadolu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha