Jumapili 3 Agosti 2025 - 15:31
Katika Mazungumzo na Wataalamu Kulichambuliwa: Burudani Zenye Madhara Katika Mazingira ya Mitandao / Tuitazame Kwa Uzito Hatari ya Uraibu wa Mitandao!

Hawza/ Burudani zilizopo katika mazingira ya mitandao ingawa zinaweza kuzingatiwa kama fursa, bila shaka zina madhara na athari zisizofaa ambazo matokeo yake yanaweza hata kusababisha hatari ya uraibu wa mitandao.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, wakati zinapozungumziwa kazi za vyombo vya habari vya kisasa, hasa katika mazingira ya mitandao, moja ya mambo muhimu na lenye matumizi makubwa ni suala la utengenezaji wa burudani, kwa kuwa moja ya majukumu ya vyombo vya habari katika zama za kisasa ni kutoa burudani.

Burudani Katika Mitandao – Faida na Hasara

Inapaswa kufahamika kwamba kinachokusudiwa kwa burudani katika mazingira ya mitandao ni uundaji na utoaji wa maudhui na shughuli mbalimbali zenye mvuto na zenye kufurahisha kwa watumiaji katika majukwaa ya mitandaoni. Hii inajumuisha michezo ya mtandaoni, video na maudhui ya picha kama vile vipande vya vichekesho, vya kielimu, filamu na mfululizo wa vipindi, pamoja na shughuli katika mitandao ya kijamii. Mitandao yenyewe, kwa kuwa na uwezo kama vile kushirikiana picha na video, kuchati na kufuatilia watu, inahesabika kama aina ya burudani.

Aidha, podcasti na maudhui ya sauti, maduka ya mtandaoni na ununuzi, pamoja na maudhui ya kielimu yenye kufurahisha pia ni sehemu ya burudani hii, kwa kuwa katika dunia ya sasa, hasa kujifunza kupitia video zenye mvuto, michezo au programu za tofauti, ina matumizi mengi.

Hadithi za Burudani Zenye Faida na Madhara

Mohammadreza Salmani, mtafiti katika nyanja ya vyombo vya habari na mawasiliano, kwa kuashiria kuwa ingawa mtandao umeongeza kiwango cha mawasiliano, pia umepelekea kuongezeka kwa umbali baina ya wanakaya, alisema:
"Burudani za mtandao endapo zitakuwa katika njia ya kukuza na kuinua utamaduni wa mtu na familia, ni zenye thamani. Lakini pale zinapotumika kupoteza muda, haziwezi kuzingatiwa kama chombo chenye faida, na kwa hivyo madhara ya eneo hili yanapaswa kufahamika vyema na kuepukwa."

Aliongeza: "Ukweli ni kwamba leo hii watu wengi wana uwepo wa kikamilifu katika mtandao na mtandao unacheza nafasi muhimu katika maisha yao, hali ambayo imewafanya watu kuzama katika mazingira haya na kutokuwa na umakini kwa familia. Kwa hakika, pale kila mtu anaposhughulika na mtandao, moja ya vipengele muhimu zaidi vya mawasiliano na mazungumzo katika familia vinapotea, na watoto kila siku wanazidi kujitenga na familia, hususan wazazi wao, na kuzama katika mazingira haya, jambo linaloongeza hatari.

Pia alibainisha kuwa: Mtandao katika wakati huu nyeti umewaathiri sana wanajamii hususan kizazi kipya, na umeielekeza jamii kwenye ubinafsi. Hali kadhalika, kifaa hiki na chombo hiki, endapo kitatumiwa kwa mtazamo na matumizi sahihi, kinaweza kuwa chombo cha kuimarisha mshikamano katika jamii, hususan ndani ya familia.

Tahadhari Kuhusu Madhara ya “Uraibu wa Mtandao”

Amir Tajallinia, Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Malezi katika Wizara ya Elimu, katika mahojiano kuhusu madhara ya mtandao yanayowatishia watoto, alisema:
"Siku hizi, tishio kubwa zaidi linalowakabili wanafunzi ni kutumia muda mwingi kupita kiasi katika mtandao, jambo linalotutia wasiwasi sana sisi kama viongozi wa elimu na pia wazazi, huenda tafsiri ya tatizo hili kwa sentensi moja ni uraibu wa mtandao."

Kuhusu iwapo kuna takwimu za wastani wa muda wanafunzi wanatumia katika mtandao, alisema: Kwa sasa hatuna takwimu maalumu kuhusu ni saa ngapi kila mwanafunzi hutumia mtandaoni kwa siku, lakini tunajua matumizi ya mara kwa mara yana madhara mengi. Mfano, suala muhimu ni muda wa wanafunzi, ambao muda wao wa thamani unapotea kwa kutumia masaa mengi kwenye mitandao, huku wazazi wakitarajia muda huu utumike kwa kazi muhimu na zenye faida. Mbali na kupoteza muda, kutumia mtandao kupita kiasi kunasababisha madhara ya kimwili kama vile kutokufanya mazoezi na unene, na zaidi ya hapo, matatizo makubwa ya uti wa mgongo na kudhoofika kwa uwezo wa kuona.

Mkurugenzi huyu pia alibainisha kuwa: Ni muhimu kufahamu ni vitu gani wanafunzi wanaangalia katika mitandao, jambo ambalo linawatia wazazi wasiwasi Ddniani kote, hata katika nchi zilizoendelea, zimetungwa mbinu za kudhibiti na kuweka mipaka kwa watoto ili kuwazuia kuhusiana na madhara ya kijamii.

Suluhu za Kuepuka Madhara

Kwa mujibu wa wataalamu, suluhu za kuepuka madhara haya zinajumuisha:

Kuweka ratiba maalum za matumizi ya mitandao kwa watoto na vijana.
Kuongeza mawasiliano ya kifamilia na kushirikiana katika shughuli za pamoja zisizo za mitandao.
Kuelimisha watoto juu ya madhara ya uraibu wa mitandao.
Kuweka vikwazo na udhibiti katika maudhui wanazopitia watoto mitandaoni.

Mtandao unaweza kuwa chombo cha kujifunza na kuendeleza maendeleo, endapo utatumika kwa usahihi. Lakini bila mpango na udhibiti, unaweza kuwa chanzo cha madhara makubwa ya kifamilia, kijamii na kiafya.

Alibainisha pia kuwa kadri tunavyoweza kuingiza furaha, uchangamfu, uhamasishaji, shughuli na kutumia muda pamoja na familia katika ratiba za watoto na vijana, mambo haya ni yenye thamani zaidi na kwa namna fulani yanachukuliwa kama njia za kinga zinazosaidia kuwazuia wanafunzi wasizame kupita kiasi katika mitandao ya kijamii.

Hakuona ni jambo la busara kupiga marufuku kabisa matumizi ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii kwa wanafunzi, bali alisisitiza haja ya kuweka itifaki na kanuni mahsusi kwa ajili ya watoto ambazo zitakuwa na mipaka.

Kwa mfano, je, mwanafunzi anaruhusiwa kumtumia mwalimu wake ujumbe wakati wowote wa usiku na mchana? Je, katika mitandao ya kijamii, kila mtu anayetaka kuwasiliana nawe unapaswa kumpa ruhusa? Au je, una uhakika na utambulisho halisi wa mtu huyo?

Alisema masuala haya yote yanapaswa kufundishwa kwa wanafunzi wetu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha