Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, wananchi wa New York na New Zealand katika maandamano yao, walidai kusitishwa mara moja mauzo ya silaha za kila aina kwa Israel, kwani jambo hili ni kuingilia moja kwa moja katika mauaji ya halaiki ya watu wa Ghaza.
Shirika la Habari la Wafa (Habari za Palestina) limeripoti kuwa, mbali na New York, mji wa Auckland pia ulikuwa shahidi wa maandamano na mikusanyiko ya wananchi. Maandamano haya tangu kuanza kwa vita vya karibuni vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza yamekuwa miongoni mwa mikusanyiko mikubwa zaidi.
Kwa mujibu wa ripoti, huku polisi wa eneo wakikadiria idadi ya waliohudhuria kuwa 20,000, lakini walioshiriki walikuwa 50,000. Washiriki wakiwa na bendera za Palestina mikononi mwao walilaani jinai za utawala katili wa Kizayuni.
Bwana Aram Rata, mmoja wa waandaaji na viongozi wa maandamano haya huko New Zealand, ameviambia vyombo vya habari: “Umakini huu mkubwa ni ishara ya ukuaji wa fikra katika jamii ya New Zealand.” Kulingana na ripoti hii pia, Waziri Mkuu wa New Zealand katika hotuba yake amezielezea hatua za Israel kuwa za kutisha mno.
Chanzo: Dearborn
Maoni yako