Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, muungano wa kibinadamu wa "Flotilla Freedom" unaofanya kazi kusaidia Ghaza, ulikuwa ukijaribu kuvunja vizuizi vya chakula Ghaza vilivyowekwa na Israel, Meli ya Hanzala yenye msaada wa kibinadamu ilikuwa ikielekea Ghaza kwa lengo hili.
Wakazi wa meli ya Hanzala walikuwa wametangaza mapema kupitia akaunti yao ya X kwamba iwapo Israel itawakamata, wataanza mgomo wa kula.
Hata hivyo, ripoti zinaonesha kuwa Israel mhalifu imeikamata meli hii, wanasheria wa watu waliokuwa ndani ya meli hiyo walitangaza kuwa watu hao ni ishirini na mmoja, wakiwemo wabunge wawili kutoka Ufaransa na waandishi wa habari wawili wa Algeria.
Shirika la kisheria la "Adalah" lilitangaza kuwa mawakili wa shirika hilo waliwasilisha maombi mengi ya kukutana na waliokamatwa katika meli hiyo, lakini licha ya kuwa kukutana na kupatiwa ushauri wa kisheria ni haki halali ya watu hao, upande wa jinai wa Israel uliwazuia kufanya hivyo.
Shirika la "Adalah" lilikazia kuwa harakati ya watu hao ilikuwa halali na ya amani kabisa, Meli hiyo ilikuwa ikijaribu tu kuvunja vikwazo vya jeshi la Israel huko Ghaza na kufikisha kiasi kidogo cha misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Palestina.
Chanzo: Shirika la Habari la France 24
Maoni yako