Alhamisi 31 Julai 2025 - 12:33
Baraza la Wanazuoni Waislamu wa Lebanon limetoa wito wa kunyang'anywa silaha adui wa Kizayuni (Israeli)

Hawza/ Baraza la Maulamaa wa Kiislamu Lebanon limetoa wito wa kunyang'anya silaha adui Muisraeli, ambaye amepora ardhi ya safari ya “Isra na Miiraj” huko Palestina

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, Baraza la Wanazuoni Waislamu wa Lebanon, katika kikao chake cha kila mwezi kilichohudhuriwa na Sheikh Muhammad Abu al-Qatta’, Mratibu Mkuu wa Baraza na mlezi wa Jumuiya ya Wahubiri, limetoa wito wa kuondolewa silaha za adui wa Kizayuni ambaye amepora ardhi ya safari ya "Isra na Miraj" huko Palestina.

Sheikh Abu al-Qatta’ alibainisha kuwa Waislamu, bila kujali tofauti za madhehebu yao, wameunganishwa kwa misingi ya dini moja, Hivyo basi, juhudi zao zinapaswa kuelekezwa katika yale yanayounganisha kauli zao, yanayounganisha juhudi zao, na yanayodumisha mshikamano wao ili waweze kukabiliana na adui yao.

Sheikh Abu al-Qatta’ alisema: “Tunasema kwa sauti ya juu kuwa Israel, ikisaidiwa na Marekani na jumuiya ya kimataifa, inapigana nasi kwa mshikamano, Hebu tuache kushambulia wapiganaji wa jihadi na kuwapangia njama, badala yake tuungane kwa kuwaunga mkono na kupigana kwa mshikamano dhidi ya maadui, hususan kwa kuwa vita vya karibuni dhidi ya Waislamu na jibu kali na linalostahili lilo tolewa kwa uvamizi huo, limemfanya adui kufikiria mara elfu kabla ya kuanzisha uvamizi mpya, kwani kwa macho yake mwenyewe aliona kuwa jibu lilikuwa ‘jicho kwa jicho’.”

Kwa upande mwingine, baraza hili limekataa waraka wa Kimarekani uliokuwa na masharti ya Israel, na limeutaja kuwa ni ukiukaji wa mamlaka ya taifa na ni dharau kwa heshima ya Walebanon wote, Waislamu na Wakristo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha