Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kufuatia kifo cha Muhammad Rastmalu, mwandishi wa habari wa shirika hilo, Ayatollah Arafi ametoa ujumbe wa rambirambi ambao maandishi yake ni kama ifuatavyo:
Bismillahir Rahmanir Rahim
إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّا إِلَیْهِ رَاجِعُونَ
Kumpoteza mwandishi wa habari mwenye juhudi na mnyenyekevu, ndugu Muhammad Rastmalu baada ya kipindi cha kustahimili maradhi, kumeleta huzuni kubwa.
Natoa mkono wa pole kwa familia tukufu ya marehemu, marafiki na jamaa, hususan jamii heshimika ya waandishi wa habari wa mkoa wa Qom na zaidi hasa wenzake wa karibu katika shirika la habari la Hawzah. Namwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Maghfirah na Upendo, amnyanyulie daraja zake na amshushie rehema pana za Mwenyezi Mungu, na kwa waliobaki awape utulivu wa moyo uliounganishwa na malipo makubwa na ya kudumu.
Alireza Arafi
Mkurugenzi wa Hawza Iran
Maoni yako