Kwa mujibu wa taarifa ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hassan Mousavi, Rais wa Jumuiya ya Kisheria ya Waislamu wa Kishia wa Jammu na Kashmir, katika tamko lake rasmi amesisitiza kuwa kitendo hiki kilichofanywa na chombo cha habari cha “India TV” ni cha kudhalilisha na kuchochea chuki dhidi ya Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Hosseini Khamenei, na ni sehemu ya njama za makusudi za maadui wa Uislamu na umma wa Kiislamu, ambazo haziwezi kukubalika kwa namna yoyote.
Ameonyesha masikitiko na wasiwasi mkubwa kuhusu kitendo hiki cha aibu cha vyombo vya habari, akibainisha kuwa vitendo vya aina hii si udhalilishaji wa utu wa Ayatollah Khamenei pekee, bali ni dharau kwa umma wa Kiislamu na kwa mhimili wa mapambano ya ukombozi; lengo kuu likiwa ni kudhoofisha mshikamano wa Waislamu na kueneza fitna na mgawanyiko.
Akiendelea mazungumzo yake ameongezea kuwa: vitendo vya aina hii vimepangwa kwa makusudi ili kutekeleza malengo ya mabeberu na uzayuni, na vinapaswa kukabiliwa kwa majibu makali ya kijamii na ya kisheria, wajibu wa viongozi wote husika ni kuwa na hisia za haraka kuhusu suala hili na kuchukua hatua madhubuti bila kuchelewa.
Rais wa Jumuiya ya Kisheria ya Waislamu wa Kishia wa Jammu na Kashmir, sambamba na kutoa wito wa kuomba msamaha rasmi na wa hadharani kutoka kwenye vyombo hivyo, ameonya kuwa iwapo havitakiri kosa na kuomba msamaha, jumuiya yake itahifadhi haki yake ya kuandaa maandamano ya amani, na kwamba jukumu la matokeo ya kutojali kwa vyombo vya habari litakuwa juu yao.
Mwanazuoni huyu mashuhuri wa Kashmiri, pia amewataka wanazuoni, wasomi, na taasisi zote za kidini na kijamii kuvunja ukimya na kwa sauti moja kumuunga mkono Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kutetea nafasi ya juu ya uongozi wa Wilaya, kwa kuchukua msimamo wa pamoja na thabiti.
Katika hitimisho la tamko lake, amesisitiza kuwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu si kiongozi wa taifa la Iran pekee, bali ni alama ya mapambano na matumaini kwa wote wapenda uhuru ulimwenguni, na kwamba kila aina ya udhalilishaji dhidi yake ni dharau kwa mambo matukufu na thamani za kibinadamu, ambazo zitakabiliwa na azma thabiti ya umma wa Kiislamu.
Maoni yako