Alhamisi 17 Julai 2025 - 00:14
Mshindi wa Mashindano ya Quran Tukufu afariki dunia

Hawza/ Ibrahim Sow raia wa Ivory Coast na mshindi wa mashindano ya Qur'ani tukufu mwaka 2024 amefariki dunia.

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, Ibrahim Sow raia wa Ivory Coast na mshindi wa mashindano ya Qur'ani tukufu mwaka 2024 amefariki dunia.Taarifa kutoka vyombo mbalimbali Nchini Ivory Coast zimethibitisha hilo jana 15 July 2025.

Ibrahim Sow aliwahi kushiriki Mashindano makubwa ya Quran ya Afrika yanayondaliwa na Taasisi ya Alhikma Foundation 2024 na kuibuka Mshindi mdogo zaidi katika uwanja wa Mkapa jiji Daresalam, mgeni rasmi wakati huo alikuwa ni Raisi wa Zanzibar na Mwenyekeiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Husein mwinyi.

Mshindi wa Mashindano ya Quran Tukufu afariki dunia

Mwaka 2024 wakati Ibrahim Sow aliposhiriki katika mashindano ya Qur'ani ya kimataifa nchini Tanzania

Ukiachilia mbali mashindano hayo, Ibrahim Sow pia aliwahi kushiriki katika mashindano makubwa zaidi ya Kimataifa ya Quran yaliyofanyika jijini Dubai manamo mwaka 2023.

Mshindi wa Mashindano ya Quran Tukufu afariki dunia

Kumbukumbu ya mwaka 2023 wakati Ibrahim Sow aliposhiriki mashindano ya Qur'ani kimataifa jijini Dubai

Katika moja ya tovuti maarufu sana nchini humo imenukuu maneno yafuatayo:

Hāfiz Ibrahim Sow, bingwa wetu kijana aliyetunukiwa kumbukumbu na Mwenyezi Mungu, mtoto mwenye fahari wa Ivory Coast, Ibrahim alijitokeza kwa umahiri wake katika usomaji na kuhifadhi Qur'an Tukufu, na hivyo akapata heshima ya kuitwa bingwa wa Afrika.

Mwaka 2025, alipata fursa ya kipekee ya kutekeleza ibada ya Hajj, akitembea katika ardhi iliyobarikiwa, akiwa miongoni mwa vijana wadogo zaidi katika msafara wa Waislamu kutoka Ivory Coast, alionesha mfano wa imani, unyenyekevu, na nuru ya kizazi kizima, kuondoka kwake kumetuacha na nyoyo zilizojaa huzuni, lakini tunakubali kwa utiifu mapenzi ya juu kabisa ya Allah.

"Sisi sote ni wa Allah na kwake tutarejea"

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha