Jumanne 9 Septemba 2025 - 15:20
Sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume wa Uislamu (saww) yafanyika Tbilisi

Hawza/ Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume wa Uislamu (saww), sherehe tukufu ilifanyika mjini Tbilisi, mji mkuu wa Georgia. Katika sherehe hii iliyoandaliwa kwa ubunifu wa Idara ya Waislamu wa Georgia na katika muktadha wa Wiki ya Umoja, wazungumzaji walieleza vipengele vya kimaisha na mafundisho ya Mtume Mtukufu (saww).

Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa elfu moja na mia tano wa kuzaliwa Mtume wa Uislamu, Bwana wetu Muhammad (saww), sherehe tukufu ilifanyika katika mji wa Tbilisi, mji mkuu wa Georgia. Hafla hii iliandaliwa kwa ubunifu wa Idara ya Waislamu wa Georgia nzima na kuhudhuriwa na kundi la wanazuoni wa kidini, watu mashuhuri wa kijamii na wanadiplomasia wa kigeni.

Sherehe ilianza kwa kisomo cha aya tukufu za Qur’ani al-Karim iliyosomwa na qari Haji Rahid Karimov, kisha wahusika wa kidini na viongozi mbalimbali akiwemo Sheikh wa Idara ya Waislamu wa Georgia, Haji Faiq Nabiyev, maftihi wa mashariki na magharibi mwa Georgia, mwakilishi wa Shirika la Serikali la Masuala ya Kidini la Georgia, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Mustafa Husseini Nishaburi – Mkurugenzi wa Kituo cha Qur’ani kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na Mahmoud Gol – mshauri wa kidini wa ubalozi wa Uturuki mjini Tbilisi, walihutubia.

Katika sehemu ya mkutano huu, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Husseini Nishaburi katika hotuba yake aligusia mambo makuu na risala za Mtume wa Uislamu (saww) na kuyabainisha kama ifuatavyo:

1- Kuunganisha makabila na dini mbalimbali kuzunguka mhimili wa haki na maadili.

2- Kuimarisha uhusiano wa kimaadili na kiimani baina ya wanadamu.

3- Kuinua akili na fikra za mwanadamu.

4- Kuendeleza njia ya kutafuta uadilifu na kushikamana na maadili.

5- Kuendeleza mafundisho kama vile mapenzi na huruma hata kwa washirikina.

6- Kuwajibika kwa mwanadamu mbele ya viumbe wengine.

7- Kuendeleza mwenendo wa kiroho kuanzia Nabii Adam hadi Nabii Isa (as) hadi mwisho.

Wazungumzaji wengine pia, sambamba na kutoa pongezi za kuzaliwa kwa Mtume wa Uislamu (saww), walijadili vipengele vya maisha yake, sifa zake za maadili na misingi ya dini ya Uislamu, vilevile mwishoni, wageni waliwasilishiwa kwa muhtasari yaliyozungumzwa kwa lugha ya Kiingereza.

Sherehe hii iliyoandaliwa katika muktadha wa “Wiki ya Umoja” ilihitimishwa kwa uimbaji wa qasida za maulidi na kasida za kidini kumuelezea Mtume wa Uislamu (saww) uliofanywa na mwimbsji wa Ahlul-Bayt, Saidi Hassan.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha