Jumanne 9 Septemba 2025 - 14:57
Harakati ya Tauhidi ya Kiislamu: Adui ameshindwa vibaya mbele ya azma na kujitolea kwa Palestina

Hawza/ Harakati ya Tauhidi ya Kiislamu nchini Lebanon imetoa pongezi kwa mapigo makali na ya kuumiza ambayo adui wa Kizayuni anaendelea kuyapokea kutoka kwa wapiganaji mashujaa wa muqawama.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, harakati hiyo katika tamko lake imesema kuwa mapigo hayo makali na ya kudumu ambayo adui wa Kizayuni amepokea kutoka kwa wapiganaji mashujaa wa muqawama, katika pambano kubwa la kihistoria ambalo wananchi wa Palestina—iwe Ghaza iliyojeruhiwa au Quds na Ukingo wa Magharibi—wamo ndani yake, ni jambo la pongezi.

Harakati hiyo ikaongeza: Katika saa chache zilizopita, tumeshuhudia kuuawa kwa Wazayuni kumi, kwa kukiri kwao wenyewe, kupitia shambulizi la risasi lililofanywa na vijana wawili Wapalestina katika operesheni maalumu ndani ya kituo kikuu cha mabasi kaskazini mwa Quds iliyokaliwa kwa mabavu, pamoja na mlipuko wa bomu ndani ya tanki la jeshi la uvamizi kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza.

Harakati ya Tauhidi ya Kiislamu ikabainisha kuwa, licha ya mazingira tata ya kiusalama, mamia ya vituo vya upekuzi vya Kizayuni na mashirikiano ya kiusalama, adui amepata pigo kubwa la mauti, na mbele ya azma na kujitolea kwa waaminifu ambao ushindi umeandikiwa kwao, ameshindwa kwa njia ya fedheha; kwa sababu wao ni watu wasiojua maana ya kurudi nyuma au kushindwa.

Harakati hiyo ikaendelea kusisitiza: Wamekuwa kielelezo cha kuigwa na mataifa katika msimamo wa kujikomboa na kupata uhuru. Umoja wa kihistoria na kijiografia ambao taifa hili linaamini ndani yake katika Ukingo wa Magharibi, Ramallah, Quds, Ghaza na kila kipande cha ardhi ya Palestina, ni wenye nguvu zaidi kuliko udikteta wa Trump na jinai za Netanyahu, na kubwa zaidi kuliko kila njama na ushirikiano wa wasaliti katika ardhi na maeneo yetu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha