Jumanne 9 Septemba 2025 - 14:50
Kughafilika na kukosekana kwa umoja wa Waislamu ndiko kunakoongeza jinai za utawala wa Kizayuni

Hawza/ Mufti wa Ahlus-Sunna wa Jamhuri ya Iraq amesisitiza kuwa Waislamu leo wamelala usingizi wa kughafilika, na utawala wa Kizayuni unatumia hali hii kuendeleza jinai zake.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Shaykh Mahdi al-Sumaida‘i, Mwenyekiti wa Dar al-Ifta Iraq, Jumatatu tarehe 17 Shahrivar 1444 katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 39 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu, alisema kuwa Mtume wa Uislamu (s.a.w.w) amesema: “Damu ya kila Muislamu ni haramu kwa Muislamu mwenzake.” Hata hivyo, tunaona jinai zisizo na idadi kutoka kwa adui Mzayuni huko Ghaza na sehemu nyingine ulimwenguni, lakini cha kusikitisha hakuna sauti kutoka kwenye nchi nyingine.

Mufti wa Jamhuri ya Iraq aliendelea kwa kusisitiza kuwa hivi sasa umma wa Kiislamu uko katika hali ngumu, akabainisha: Ni lazima Waislamu wote kwa kauli moja na kwa mshikamano wa pamoja wasimame dhidi ya adui, kwani adui kwa majivuno yake yasiyo na msingi amejipa ujasiri wa kuwatishia viongozi na wakuu wa nchi za Kiislamu, na hii ni kwa sababu mataifa yamezama katika usingizi mzito.

Akiashiria hali ya Waislamu kutofautiana na kugeukiana wenyewe kwa wenyewe hadi kuuwana, alisema: Hali hiyo imewapa kisingizio Wamagharibi kudai kwamba Waislamu wanajiharibu wao kwa wao.

Al-Sumaida‘i aliendelea kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awaamshe Waislamu kutoka usingizi wa kughafilika, ili waweze kubeba jukumu zito lililowekwa mabegani mwao. Pia alimwomba Mwenyezi Mungu kuufanikisha mkutano huu katika malengo yake, na umoja urejee tena kwa Waislamu wote ili wawe wamoja na wameshikana.

Mwisho, Mufti wa Ahlus-Sunna wa Jamhuri ya Iraq alisisitiza: Tunapaswa kusema “Ndiyo” kwa umoja wa Waislamu, na kusema “Hapana” kwa ubeberu wa kimataifa na kwa Wamagharibi wenye kiburi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha