Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Sayyid Abdulqadir Alusi, Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Ribat Muhammadi Iraq, katika Mkutano wa 39 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu uliofanyika leo tarehe 17 Shahrivar katika Ukumbi wa Mikutano ya Marais, akitoa pongezi kwa maadhimisho ya kuzaliwa Mtume mtukufu wa Uislamu (s.a.w.w), alisema: Kuandaliwa kwa mikutano na makongamano kama haya ni jambo lenye thamani kubwa na lenye manufaa; Waislamu leo, kama ilivyokuwa hapo awali, wanahitajia mazungumzo ya kimaendeleo na mawasiliano yenye malengo baina ya umma wa Kiislamu, tawala za Kiislamu na hasa wasomi na wanazuoni.
Akaendelea kusisitiza: Wanazuoni wote waliopo katika Mkutano wa Umoja wa Kiislamu wanapaswa kutumia jitihada zao zote ili mkutano huu mkubwa ugeuzwe kuwa umoja wa kisiasa na kivitendo.
Mwenyekiti huyo wa Baraza la Wanazuoni wa Ribat Muhammadi Iraq akibainisha ulazima wa kutumia ipasavyo nyenzo zote zilizopo kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa Umoja wa Kiislamu, aliongeza: Tunapaswa katika Mkutano wa Umoja wa Kiislamu kufanya kazi ya kuutangaza na kueneza Uislamu.
Mwisho, Sayyid Alusi, kwa kurejea ushindi wa Iran katika vita vya siku 12, alibainisha: Wananchi wa Iran kwa kusimama pamoja na uongozi wao waliweza kumshinda adui, na sisi wanazuoni tunapaswa kuunga mkono mkutano huu ili tufikie umoja wa kweli.
Maoni yako