Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Sheikh Hassan Muhammad Qasim, Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Palestina, katika ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Thelathini na Tisa wa Umoja wa Kiislamu uliofanyika leo tarehe 17 Shahrivar katika Ukumbi wa Mikutano ya Marais, alisema: Sasa wakati umefika wa kujiuliza je, kwa hakika mnamfuata Mwenyezi Mungu?
Akaendelea kusema: Palestina ni moyo wa umma wa Kiislamu, na Wamagharibi kwa kuzingatia jambo hili, kwa ajili ya kuleta mgawanyiko na kuuangamiza ulimwengu wa Kiislamu, wameulenga moyo wa umma wa Kiislamu.
Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Palestina alisisitiza: Leo, karibu na Ghaza kuna nchi za Kiislamu, lakini wananyima watu wanyonge wa Ghaza maji na mkate, na wameziziba mipaka yao dhidi ya watu hawa. Je, hao ni Waislamu? Je, nchi za Kiislamu haziwezi kupeleka maji kwa watu wa Ghaza? Nchi ambazo zinalala juu ya bahari ya mafuta haziwezi kupeleka chakula kwa Waislamu?
Sheikh Hassan Muhammad Qasim mwishoni, huku akibainisha kuwa: Hatutaki kitu kisichowezekana kutoka kwenu; tunachotaka ni kupatiwa mkate, dawa na maji kwa wakaazi wa Ghaza. Je, hili ni ombi kubwa mno kutoka kwa ulimwengu wa Kiislamu? Alisisitiza kwa kusema: Ewe umma wa Kiislamu! Iungieni mkono Palestina, kwani iwapo Ghaza itaanguka, hakika nanyi mtaanguka, kwa sababu nchi za Kiislamu zina uhusiano wa karibu baina yake.
Maoni yako