Jumatano 30 Julai 2025 - 07:29
Elimu ya “chumba cha baridi” haimjengi mwanadamu

Hawza/ Mtukufu Ayatollah Jawadi Amuli alibainisha kuwa: “Kile kilichopo leo katika baadhi ya jamii za kielimu za vyuo vikuu ni elimu iliyokufa na ya chumba cha baridi; elimu hii ya chumba cha baridi haiwalei wanazuoni wakubwa, na wala haimjengi mwanadamu, bali ni chombo tu.”

Kwa mujibu wa ripoti ya  Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Ayatollah Jawadi Amuli katika kikao chake na kundi la walimu wa Chuo Kikuu cha Kashan, huku akisisitiza umuhimu wa kuunganisha Hawza na Chuo Kikuu, alibainisha kuwa: “Muda wa kuwa uhusiano kati ya mjuzi na elimu haujafafanuliwa ipasavyo, muungano wa Hawza na Chuo Kikuu pia hautatimia. Elimu ni hakika ya pembetatu; upande mmoja umeunganishwa na mwanzo – ni nani aliyeumba kinachojulikana? Upande wa pili umeunganishwa na mwisho – kwa nini kiliumbwa? Na upande wa katikati – ni nini hasa?”

Yeye aliendelea kusema: “Elimu ni nuru ambayo Mwenyezi Mungu huipandikiza moyoni mwa yule amtakaye. Lakini kilichopo leo katika baadhi ya jamii za kielimu za vyuo vikuu ni elimu iliyokufa na ya chumba cha baridi; elimu hii haiwalei wanazuoni wakubwa; elimu hii haimjengi mwanadamu, bali ni chombo tu. Tunapaswa kuwa na elimu hai, ya kiushuhuda na yenye kuhuisha; elimu ambayo kinachojulikana kwake si takwimu za kiakili tu bali ni hakika yenye uhusiano na uwepo na Mwenyezi Mungu.”

Mtukufu Ayatollah Jawadi Amuli alisema: “Hatua ya kwanza kwa mwanadamu ni maarifa ya nafsi; mwanadamu akijua kwamba yeye ni hakika hai, na akajua ametoka wapi na anakwenda wapi, hataisahau nafsi yake tena. Atakapofahamu kwamba ‘mimi nipo, nipo, nipo’ na siwezi kuoza, bali kwa kifo ninatoka katika ganda, ndipo atakapofikia elimu ya kiushuhuda. Maarifa haya ni zawadi kubwa kwa mwanadamu; mwanadamu wa namna hii hapotei njia wala hazuii njia ya mtu mwingine.”

Yeye aliongeza kwa kusema: “Uhuru katika mantiki angavu ya Hadhrat Amir (as) ni kuachana na matamanio na matarajio ya nafsi, sio kuachwa huru katika tamaa za anasa. Kama ilivyo mfumo wetu wa mmeng’enyo una tamaa, lakini si kila chakula kinatufaa, vivyo hivyo matamanio ya mwanadamu lazima yapimwe kwa maumbile na hakika yake.”

Mtukufu Ayatollah Jawadi Amuli alisema: “Kila mandhari, kila muziki au kila mwenendo unaoupendelea si lazima uwe na manufaa kwetu, kwani sisi ni viumbe wenye mipaka na hatuwezi kuwa na matamanio yasiyo na kikomo, uhuru wa mja upo katika ukamilifu wa uabudifu wake.”

Mwanazuoni mkubwa huyu alibainisha kuwa: “Ghera ni miongoni mwa fadhila bora zaidi za kinafsi; ghera si katika masuala ya kifamilia pekee; ghera ni neno lenye kutokana na vipengele vitatu mahsusi:
Kwanza, mwanadamu asivunje heshima ya mwingine - kutokutazama wasio maharimu, kutojinyoosha kwa mali ya umma, na kutovamia haki za taifa, vyote hivi ni mifano ya ghera.

Pili, mwanadamu mwenye ghera haruhusu heshima na hifadhi yake ivunjwe, kama alivyoeleza katika maneno yenye mwanga Amirul M'uminin:

«رُدُّوا الْحَجَرَ مِنْ حَیْثُ جَاءَ»
"Rudisheni jiwe lilipotokea,” 


na akasema:
«لَا یَمْنَعُ الضَّیْمَ الذَّلِیلُ» 
“Udhalili wa kupokea dhulma haukubaliwi ila na dhalili.”

Na kipengele cha tatu: Mwanadamu lazima awe mjuzi wa mipaka; mwanadamu asipofahamu mipaka yake, hawezi kupima kwamba wapi amevuka mipaka na wapi mipaka yake imevunjwa, vipengele hivi vitatu vikikusanyika, mtu huyu anakuwa ni mwenye ghera.

Mwisho wa mkutano huu, aliwataka walimu wa vyuo vikuu kuwa watu wa vitendo na unyenyekevu, na akabainisha kuwa: “Popote mjuzi mwenye vitendo, mnyenyekevu na mwenye maana atakapokuwepo, mioyo huvutiwa, hatujihitaji tishio la nguvu ili kuivuta mioyo, bali tunahitaji ukweli na nuru ya elimu.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha