Jumamosi 21 Februari 2026 - 12:18
Luninga kubwa zaidi barani Ulaya yatangaza kuanza kwa Ramadhani

Hawza/ Luninga kubwa na maarufu zaidi ya matangazo ya kidijitali barani Ulaya imewashwa na kupambwa kwa taa maalum ili kuadhimisha kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mwangaza huo ulioendana na kuanza rasmi Ramadhani duniani, ukiwasilisha ujumbe usemao kwamba; "mwezi huu mtukufu umeanza kwa Waislamu wote ulimwenguni".

Skrini hiyo kubwa sana iliyopo katikati ya eneo la Piccadilly Circus huvutia takribani wageni milioni 100 kila mwaka na inachukuliwa kuwa mojawapo ya majukwaa yanayoonekana zaidi ya matangazo duniani. Waandaaji wa tangazo hilo walisema kuwa; ujumbe huo ni ishara ya utofauti na dhamira ya London ya kusherehekea matukio ya umma kwa ushirikishwaji mpana.

Sambamba na tukio hilo, maonyesho ya kwanza ya sanaa ya dini mbalimbali yameandaliwa katikati ya London, yakifadhiliwa na Trocadero London pamoja na Taasisi ya “Ramadan Tent Project” (Mradi wa Hema la Ramadhani). Waandaaji wamechagua njia maalum jijini humo ambapo kwa muda wa mwezi mzima wataandaa futari katika migahawa, kumbi za chakula na sehemu maarufu za kimataifa za vyakula.

Chanzo: 5Pillars

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha