Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Riyad Mansour, balozi wa Palestina, alisoma taarifa ya pamoja iliyoungwa mkono na nchi kutoka kote Ulaya, Asia Magharibi, Afrika, Asia na Amerika ya Kusini, pamoja na Umoja wa Nchi za Kiarabu na Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu.
Katika taarifa hiyo, mchakato wa hivi karibuni wa usajili wa ardhi na Israel katika eneo la Ukingo wa Magharibi ulilaaniwa, na Ukingo wa Magharibi ukatambuliwa kuwa ni sehemu ya ardhi halisi ya Palestina. Taarifa hiyo ilisema: “Hatua kama hizi zinakiuka sheria za kimataifa, zinadhoofisha juhudi za amani na uthabiti, na zinahatarisha uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano ya amani ya kina.”
Lawama hii imetolewa wakati wa kuongezeka kwa vurugu katika Ukingo wa Magharibi na Mashariki mwa Quds, ambako kuongezeka kwa operesheni za kijeshi, mauaji na kukamatwa kwa raia wa kawaida vinaendelea kufanyika kwa ukatili mkubwa.
Chanzo: EUPAC
Maoni yako