Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Allamah Hasan Zadeh (ra), akirejelea maneno ya Amirul-Mu’minin (as), anafafanua hali ya mwili na roho kama ifuatavyo:
Allamah Hasan Zadeh Amoli:
Amirul-Mu’minin (as) amesema:
“Mwili una hali sita: afya; ugonjwa; mauti; uhai; usingizi; na kuamka.”
“Na roho pia ni vivyo hivyo; basi uhai wake ni elimu yake, na mauti yake ni ujinga wake, na ugonjwa wake ni shaka yake, na afya yake ni yakini yake, na usingizi wake ni kughafilika kwake, na kuamka kwake ni kujilinda kwake (kutokana na madhambi).”
Chanzo: ‘Uyuun Masail al-Nafs’ na maelezo yake, Juzuu ya 1, uk. 95
Maoni yako