Jumapili 3 Agosti 2025 - 01:01
Khatibu wa Swala ya Ijumaa India: Kumtukana Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ni kuutukana Umma wote wa Kiislamu/ Vyombo vya habari vya India viwaombe msamaha Waislamu

Hawza/ Hujjat al-Islam Sayyid Naqi Mahdi Zaidi, katika khutba ya Swala ya Ijumaa, huku akielezea nafasi ya kipekee na yenye ushawishi ya Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei (Mola amuhifadhi), alilaani vikali kitendo cha matusi kutoka katika baadhi ya vyombo vya habari vya India na kukitaja kuwa ni matusi kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama yaShirika la Habari la Hawza, Hujjat al-Islam Sayyid Naqi Mahdi Zaidi, Imamu wa Ijumaa wa Taragra nchini India, katika khutba ya Swala ya Ijumaa, huku akielezea nafasi ya kipekee na yenye ushawishi ya Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, alilaani vikali kitendo cha matusi ya baadhi ya vyombo vya habari vya India na kukitaja kuwa ni tusi kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu.

Kiongozi Mkuu: Sura ya Kimataifa na Mwenye Kuheshimiwa na Umma wa Kiislamu

Katika hotuba yake alisisitiza kwamba Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu si tu kiongozi wa kiroho na marja’ taqlid wa Waislamu wa Kishia duniani, bali pia ana hadhi ya juu na heshima miongoni mwa mataifa ya Kiislamu na wapenda uhuru duniani kote.

Imamu wa Ijumaa wa Taragra nchini India aliongeza kuwa: Kumtukana mtu wa aina hii si suala la ndani au la kidini pekee, bali ni shambulio kwa dhamira iliyoamka na imani za kina za Umma wa Kiislamu, Ujasiri kama huu ni dharau kwa Waislamu wote duniani.

Matusi dhidi ya Kiongozi Mkuu ni mradi wa kudhoofisha jukwaa la muqawama

Akiendelea na hotuba yake, huku akichambua malengo yaliyo nyuma ya matusi haya ya vyombo vya habari, alisema kuwa; ni jitihada zilizoshindikana za kudhoofisha jukwaa la upinzani na kufifisha wimbi la msaada wa kimataifa kwa taifa dhalili la Palestina.

Leo, duniani kote, msaada kwa watu wa Palestina umekuwa harakati ya kimataifa, uongozi wa harakati hii uko mikononi mwa kiongozi mwerevu, mwenye imani na mwenye kuona mbali kama Mtukufu Ayatollah Khamenei, ni jambo la kawaida kwamba maadui wa muqawama wanahofia kuamka mataifa na wanataka kwa kushambulia hadhi ya uongozi huu, kuzuia wimbi hili.

Matusi ni ishara ya udhaifu, si ya nguvu

Mwanachuoni huyu aliendelea kusema kwamba: Makelele na uongo huu ni jitihada za kuficha ukweli ambao leo umekuwa wazi zaidi kwa mataifa yaliyoamka duniani, ukweli kwamba kilio cha Wapalestina waliodhulumiwa, sauti ya upinzani, na utu wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi umeufanya kuwa dhahiri.

Alibainisha zaidi kwamba matusi na upotoshaji kama huu si ishara ya nguvu, bali ni ishara ya udhaifu, hofu na kushindwa kisaikolojia kwa maadui wa Uislamu.

Onyo kuhusu kuporomoka kwa maadili ya vyombo vya habari nchini India

Hujjat al-Islam Naqi Mahdi aliendelea na hotuba yake kwa sauti kali na ya onyo, huku akilaani vikali mwenendo wa baadhi ya vyombo vya habari maarufu vya India kama vile "India TV" na "Hindustan Times", na kusema: India leo inakabiliwa na aibu na fedheha kubwa, na chanzo kikuu cha kuporomoka huku kwa maadili na kijamii ni vyombo vya habari ambavyo vimepoteza uhuru wao wa kitaalamu na kuwa zana za propaganda za utawala wa Kizayuni, vyombo hivi vya habari, vikipewa amri na Israel, havitasita hata kukashifu vitu vitakatifu na heshima ya kitaifa yao wenyewe.

Wito wa kuomba msamaha rasmi hadharani

Hujjat al-Islam Sayyid Naqi Mahdi akiendelea kwa kusisitiza haja ya kushughulikia kwa ukali matusi kama haya, alitoa wito wa msamaha rasmi kutoka kwa vyombo hivyo vya habari, na akabainisha kuwa: Tunataka vyombo vya habari ambavyo kwa kutusi moja ya sura kubwa za kidini na kimataifa vimejeruhi hisia za mamilioni ya Waislamu, viombe msamaha rasmi kwa sauti ile ile kubwa na kupitia majukwaa yale yale. Hatua hii ya chini kabisa inatarajiwa kuchukuliwa ili kuheshimu misingi ya kibinadamu, maadili ya vyombo vya habari, na maisha ya pamoja yenye amani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha