Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Hazm al-Asad, mjumbe wa baraza la kisiasa la Ansarullah, amesema: Awamu ya nne ya operesheni zetu za kijeshi kwa ajili ya kuunga mkono watu wa Ghaza, itazilenga kampuni zote za usafirishaji wa baharini ambazo zina mikataba na utawala wa Kizayuni, pamoja na nchi za Kiarabu! Mchakato huu utaendelea hadi pale utawala wa Kizayuni mnyanyasaji na dhalimu utakapositisha kuzingirwa kwa Ghaza, Vikosi vyetu vimeazimia kupanua operesheni zao dhidi ya adui wa Kizayuni, Wajue wote kwamba wale wanaounga mkono mauaji na njaa huko Ghaza, au hawakemei, wanashirikiana na upande wa Israel.
Akaongeza kuwa: Ni jambo la aibu na fedheha kwamba baadhi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu katika kipindi hiki zinafanya urafiki na utawala wa Kizayuni na hata kuongeza biashara zao na nchi hii.
Kabla ya hapo, Ansarullah ilitangaza kwamba meli iliyolengwa katika Bahari Nyekundu mara kadhaa ilikuwa imebeba mizigo kwa ajili ya utawala wa Kizayuni kutoka bandari za Misri na Uturuki, na ilishapewa onyo mara kadhaa.
Chanzo cha kijeshi cha Yemeni kilisisitiza kuwa: Tunatoa onyo kwa nchi zote na meli zote kwamba kwa ajili ya usalama wao na meli zao, wasifanye biashara na utawala huu wa kinyama, unyanyasaji na wa mauaji ya kimbari!
Chanzo: Shirika la Habari la Ava Press
Maoni yako