Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, hafla ya ufunguzi wa mfululizo wa vikao vya “Utafiti wa Nahjul-Balagha” ilifanyika kwa kuhudhuriwa na watafiti na wapenzi wa maneno ya Ali ibn Abi Talib (a.s), na kwa hotuba ya Reza Ustadii.
Mjumbe wa Jumuia ya Walimu wa Hawza ya Qom katika kikao hicho, kilichoandaliwa kwa lengo la kufafanua misingi ya utafiti katika Nahjul-Balagha, alichambua vipengele mbalimbali vya shakhsia ya mkusanyaji wa kitabu hicho kitukufu, pamoja na tathmini na uhakiki wa sherehe muhimu zaidi zilizoandikwa juu yake.
Kuthibitisha hadhi ya kifaqihi na kitafsiri ya Sayyid Radhi
Ayatullah Ustadi katika sehemu ya kwanza ya hotuba yake alirekebisha taswira potofu ya kihistoria kuhusiana na shakhsia ya Sayyid Radhi na kusema: Kinyume na dhana ya wengi wanaomwona Sayyid Radhi kama mshairi na mwandishi wa fasihi tu, yeye alikuwa faqihi mashuhuri na mfasiri mkubwa wa Qur’ani.
Akiashiria walimu wake katika fiqhi, fatwa zake, pamoja na uandishi wake wa tafsiri kubwa ya Qur’ani Tukufu yenye juzuu kumi, alisisitiza juu ya upeo mpana wa kielimu wa mkusanyaji wa Nahjul-Balagha.
Uhalisi wa Nahjul-Balagha na majibu kuhusiana na shubha za isnadi
Mjumbe wa Jumuia ya Walimu wa Hawza ya Qom, kwa kutegemea ushahidi wa kihistoria, alikanusha shubha zilizotolewa na baadhi ya wenye nia mbaya kwamba kitabu hicho hakihusiani na Sayyid Radhi, na akasema: Kuwepo kwa nakala za maandishi ya mkono kwa hati ya Sayyid Radhi mwenyewe hadi karne kadhaa baada ya kufariki kwake — ambazo zilishuhudiwa na wanazuoni wakubwa kama Ibn Abi al-Hadid — ni uthibitisho wa kitabu hiki.
Ayatullah Ustadi pia, akijibu shubha kuhusu “mursal” (kutotajwa kwa mnyororo wa wapokezi) katika riwaya za Nahjul-Balagha, alisema: Sayyid Radhi, kutokana na mtazamo wake wa kifasihi, aliacha kutaja isnadi; hata hivyo, wanazuoni wa baadaye kwa kuandika vitabu vya nyongeza (mustadrak), wamechambua na kubainisha isnadi za khutuba na barua zote hizi.
Tathmini ya sherehe maarufu za Nahjul-Balagha
Mjumbe wa Jumuia ya Walimu wa Hawza ya Qom, aliendelea kwa kuchambua sherehe mbili mashuhuri za wanazuoni wa Ahlus-Sunna juu ya Nahjul-Balagha, na akasema: Pamoja na kuthamini juhudi za Muhammad Abduh katika kuitambulisha Nahjul-Balagha kwenye ulimwengu wa Kiarabu, kuna ukosoaji mkubwa kuhusu mbinu yake. Kila mahali ambapo maneno ya Amirul-Muuminin (a.s) hayakulingana na itikadi za Ahlus-Sunna, aliyabadilisha au kuyaita kuwa yametungwa.
Pia kuhusu sherehe ya juzuu 20 ya Ibn Abi al-Hadid al-Mu’tazili, aliitaja kazi hiyo kuwa tajiri sana kwa upande wa fasihi na historia, lakini kwa upande wa kalamu na itikadi ina upotofu na upendeleo mkali, hivyo inahitaji kusomwa kwa mtazamo wa kina na uhakiki.
Utukufu wa maneno ya Amirul-Muuminin (a.s)
Mjumbe wa Jumuia ya Walimu wa Hawza ya Qom, huku akirejea kauli za wanazuoni wakubwa kama Mulla Sadra, alisisitiza: Maneno ya Imamu Ali (a.s) katika Nahjul-Balagha yako katika kilele cha fasaha na balagha, yakiwa daraja moja chini ya maneno ya Muumba na juu ya maneno ya kiumbe.
Maoni yako