Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mike Rok, mmoja wa washiriki katika hafla hiyo, alisema: “Ninawafamisha wote: kama hamjui Uislamu ni nini, sisi tupo hapa. Tazameni upendo huu na mshikamano huu. Jitahidini kuufahamu Uislamu wa kweli na sahihi, na uwasilisheni ujumbe wa kweli wa Qur’ani kwa njia nzuri zaidi kwa wengine.”
Kaulimbiu yetu katika Iftari hii ni: Ikiwa una uhitaji, hata kama si Mwislamu, shiriki katika meza hii ya Iftari. Tunagawana mkate mmoja vipande viwili na tunafuturu pamoja. Huu ndio mshikamano na hisia nzuri ya huruma inayotiririka miongoni mwetu.
Chanzo: GDN ONLINE
Maoni yako