Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mjumbe wa wanazuoni wa Baraza la Kulinda Katiba nchini Iran, aliendelea kusema kuwa; hata kabla ya kuzikwa Bibi Fatima Masumeh (amani iwe juu yake) katika mji wa Qom, Qom tayari ilikuwa ikitambulika kama eneo muhimu la kidini na kitamaduni, na hadi leo mji huo ni kitovu cha kueneza utamaduni wa Kiislamu na wa kidini.
Nafasi ya Qom Katika Historia
Mkurugenzi wa Hawza za Elimu ya Kiislamu, alisisitiza umuhimu na mchango wa watu wa Qom katika kuhifadhi na kuendeleza utamaduni huu wa kidini, akiongeza kuwa: Qom katika historia yake haijawahi kupotoka kutoka katika njia ya kielimu na kidini. Wakati miji mingi kama Ray au Baghdad ilitengana na mwelekeo huo kutokana na matukio mbalimbali, Qom imeendelea kusimama imara katika njia hiyo.
Aidha, aligusia nafasi maalumu ya Qom katika historia ya Uislamu na Ushia, akieleza kuwa; katika vipindi mbalimbali vya historia, Qom imekuwa ikitambulika kama kituo muhimu cha kielimu na kidini kwa Waislamu, hususan Mashia. Katika zama tofauti, mji huo haujawahi kukengeuka katika mawasiliano yake ya kielimu na kidini, jambo linaloufanya utambulike na kutofautiana na maeneo mengi mengine.
Maoni yako