kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Khatibu wa Ijumaa ya Qom, Ayatollah Alireza A'rafi, alisema kuwa maadui na wanafiki wafahamu kuwa wamepiga mahali pasipo sahihi, wamefanya makosa ya kimkakati na kutenda jinai kubwa. Baadhi ya watu kwa urahisi wanafikiri wanaweza kutoa pendekezo la amani – lakini hawa ni watu wapumbavu, wanafiki na wenye chuki, walioingia katika tafsiri potofu ya hali halisi.
Katika hotuba ya Swala ya Ijumaa ya tarehe 30 Khordad 1404 (sawa na 20 Juni 2025), iliyofanyika katika Musalla ya Quds mjini Qom, Ayatollah A'rafi alieleza kuwa:
Mapinduzi ya Kiislamu: Mwanga katika Giza la Magharibi
"Mapinduzi ya Kiislamu yalikuwa ni kilio cha haki katikati ya giza la dunia ya Magharibi. Dunia ambayo ilikuwa chini ya buti za mabeberu na ustaarabu wa uongo na wa kimada wa Magharibi ambao uko katika hali ya kuangamia. Dunia iliyojawa na dhulma, usawa usiopo, na kuendeshwa kwa misingi ya kura ya turufu (veto) ya mataifa makubwa. Taasisi za kimataifa zimekuwa ni zana za dola za kibeberu duniani."
Historia ya Karne ya 20: Maovu ya Magharibi
Aliongeza:
"Kwa zaidi ya miaka 100, dunia imeshuhudia vita, uporaji wa mali za mataifa, ukoloni, mauaji ya halaiki, kuporwa kwa uhuru wa mataifa, na kuvamiwa kwa ardhi za Kiislamu na za Mashariki. Sera ya mabeberu ni kwamba: ima uwe upande wao, au uharibiwe kabisa – na ubaki kuwa nchi isiyo na nguvu wala mustakabali." Iran Imeinuka Dhidi ya Mfumo wa Kibeberu
Ayatollah A’rafi alisisitiza:
"Ninyi watu wa Iran mmesimama dhidi ya mfumo huu dhalimu na mumeendelea mbele kwa nguvu. Mabeberu wanataka kuwanyang’anya mafanikio haya. Lakini Iran haikubali kuwa mnyonge wala ardhi iliyoteketezwa – bali taifa huru, lenye maendeleo, na linalobadilisha mizania ya nguvu duniani. Huu ndio ujumbe na siri ya mapinduzi yenu."
Onyo kwa Umma wa Kiislamu: Msisahau Asili ya Mapinduzi
"Dada na kaka zangu, msiruhusu mtu yeyote awapotoshe kutoka katika kiini cha mapinduzi haya. Mapinduzi ya Kiislamu ni mabadiliko ya msingi katika ustaarabu wa dunia, na ni kilio cha ukombozi dhidi ya dhulma iliyofanywa kuwa jambo la kawaida. Iran imesimama imara, na itaendelea kusimama zaidi kuliko wakati wowote."
Israel si Taifa – Ni Kambi ya Kijeshi ya Magharibi
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, alisisitiza:
"Israel si dola halali wala taifa – bali ni kambi ya kijeshi ya Magharibi. Tulisema hili miaka 50 iliyopita. Wameiweka ili kuibadilisha dunia ya Kiislamu kuwa kama Syria na kuitawala. Israel ni hatari kwa Uislamu wote. Mataifa yote ya Kiislamu yafahamu: Israel ni tishio kwa kila mmoja, kwa utu wa mwanadamu, na kwa uhuru wa mataifa yote."
Maoni yako