Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza Arafi, Mkurugenzi wa Hawza za Kiislamu, wakati akilaani utawala wa Kizayuni kwa kuvunja kwa wazi kabisa mamlaka na uhuru wa Iran, pamoja na kuanzisha vita vya pande zote kwa msaada wa baadhi ya nchi za Magharibi (hasa Marekani) dhidi ya taifa la Iran linalopenda amani, alisema:
Baadhi ya raia wasio na hatia pamoja na wasomi wa kisayansi na wa nyuklia, na makamanda wa kijeshi wa Iran wameuawa kishahidi; na pia taasisi kadhaa za kiraia na miundombinu yetu vimekuwa shabaha ya mashambulizi.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza za Kiislamu aliendelea kwa kusema: Utawala huu wa kinyakuzi kwa miongo kadhaa umekuwa ukiivamia ardhi ya Palestina na mataifa ya Kiislamu, na mikono yake imejaa damu ya watu wasio na hatia. Na kama Qur'an Tukufu inavyosema:
«لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِلَّذِینَ آمَنُوا الْیَهُودَ وَالَّذِینَ أَشْرَکُوا.»
"Hakika utawakuta watu wenye uadui mkali zaidi kwa wale walioamini kuwa ni Mayahudi na washirikina." (Al-Maida: 82)
Utawala huu umetenda uadui mkubwa zaidi dhidi ya Waislamu katika historia.
Mkurugenzi wa Hawza za Kiislamu amewaomba maulamaa na watu mashuhuri wa Kiislamu na wa dini nyengine kwamba: Katika kipindi hiki nyeti na chenye umuhimu wa kihistoria, inatarajiwa viongozi wa Kiislamu na wa dini nyingine duniani kuwa Pamoja, na kulaani kwa nguvu na kwa uwazi uvamizi unaozidi kuongezeka wa utawala wa Kizayuni, wafikishe sauti ya dhulma wanayoipata watu wa Iran kwa mataifa yote, na wafanye juhudi za dhati za kuleta umoja wa kweli kwa Umma wa Kiislamu dhidi ya adui wa pamoja ambae ni utawala wa Kizayuni.
Maoni yako