Alhamisi 19 Juni 2025 - 18:41
Mpaka mwisho wa vita tupo Pamoja nanyi/ Wapiganaji jihadi wa Hawza wapo tayari kwa ajili ya kujenga nyumba Pamoja na sehemu zilizo haribiwa

Hawza/ Ayatollah Arafi amesema; sisi tupo Pamoja nanyi situ katika ujenzi bali katika majeraha yote, kuwatia moyo na kuwakingia kifua, tunayo Imani ya kweli kwamba taifa hili tukufu litafanikiwa kuupita huu mtihani mzito na wenye machungu.

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, Matini ya ujumbe wa Ayatollah Arafi Mudiri wa hawza za Qum, akiliongelesha taifa la Irani ni kama ifuatavyo:

بسم الله الرحمن الرحیم

Taifa tukufu la Irani na wananchi wake walio simama kidete dhidi ya dhulma na kupetuka mpaka kwa Wazayuni.

Katika masiku ya majeraha yanayotokana na ukhabithi wa wazayuni wauwaji wa Watoto, hawza kwa matakwa na Imani kamili imesimama Pamoja nanyi, sisi tunaamini kwamba maumivu anayo yapitia muirani mmoja ni sawa swa na maumivu wanayo yapitia wairani wote.

Leo hii pia wanajihadi wa hawaza kama ilivyo kuwa katika kipindi cha kupambana na balaa la korona walijitolea nafsi zao, kwa nia ya dhati na kuchegemea malengo ya mda mrefu ya mapinduzi ya kiislamu, wako tayari kujitolea katika Nyanja tofauti kwa ajili ya kutoa huduma kama vile kutengeneza nyumba na sehemu zilizo haribiwa, ili kushiriki nao katika jambo hili gumu na la kidugu ili kuonesha umoja na udugu wa kiislamu katika suala hili zito.

Sisi tupo Pamoja nanyi si tu katika ujenzi bali katika majeraha yote, kuwatia moyo na kuwakingia kifua, tunayo Imani ya kweli kwamba taifa hili tukufu litafanikiwa kuupita huu mtihani mzito na wenye machungu, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, na chini ya kivuli cha umoja na mshikamano wa kitaifa, sehemu zilizo haribiwa zitarekebishwa kwa hari ya hali ya juu, na huzuni zote zitabadilika kuwa ni Faraja.

Tunawaombea mashahidi wote rehema na ridhaa za Mwenyezi Mungu, na pia twaziombea familia zao zipate Subira, Pamoja na kuviombea vikosi vya jeshi la Irani viweze kupata ushindi.

Ali Reza Arafi

Mudiir wa hawza za Qum

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha