Jumamosi 24 Mei 2025 - 20:24
Tuuba Kermani; Mwanamke Mfilosofia wa Iran na Kielelezo cha Mwanamke Muislamu katika Nyanja ya Elimu na Maadili

Hawza/ Dkt. Tuuba Kermani, Profesa Mstaafu wa Kitivo cha Theolojia na Maarifa ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Tehran, kupitia jitihada zake za kielimu na malezi, si tu aling’ara katika uwanja wa Falsafa ya Kiislamu, bali pia aligeuka kuwa kielelezo cha wanawake Waislamu katika ngazi ya kimataifa. Kwa kudumisha mavazi na heshima ya Kiislamu, aliweza kubadilisha mtazamo hasi kuhusu mwanamke Muislamu wa Iran, na kusababisha kuwavutia watu wengi wasio Waislamu kuingia katika Uislamu.

Shirika la Habari la Hawza - Tuuba Kermani, mwanamke msomi na mfilosofia wa Iran, kwa bidii na sauku yake ya kujifunza elimu, aliweza kupata shahada ya juu ya "Post-doctorate" kutoka katika Chuo Kikuu cha California, na anatambulika kama mwanamke wa kwanza Mfilosofia wa Iran. Kwa miaka mingi, aliwahi kufundisha falsafa na maarifa ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Tehran na kulea wanafunzi wengi katika sekta mbalimbali za kisayansi za kibinadamu na Kiislamu.

Bi Kermani daima alikuwa akisisitiza kwamba mafanikio ya kielimu na kijamii hayana mgongano wowote na kudumisha thamani za kidini na vazi la Kiislamu. Kwa maadili yake mema, imani thabiti, na elimu yake pana, si tu katika Iran, bali pia katika vikao vya kielimu vya kimataifa, alipata heshima kubwa na hata kuwatia mshangao maprofesa wa Marekani.
Wanafunzi na wenzake wengi walimchukulia kama kielelezo cha mwanamke Muislamu wa Iran ambaye aliweza, kwa mwenendo na tabia yake, kutoa taswira chanya ya wanawake wa Iran katika kiwango cha kimataifa.

Moja ya majukumu muhimu zaidi ambayo Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyaweka juu ya mabega ya wanawake mashuhuri na wanazuoni wakike ni kuutambulisha mfano wa mwanamke Muislamu wa Iran katika dunia; jukumu ambalo Tuuba Kermani alilibeba vyema. Hadi mwisho wa maisha yake, aliendelea kuwa mfuasi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Kiongozi wake, na kwa ari na juhudi alichukua hatua katika njia ya maendeleo ya kielimu na kitamaduni ya nchi.

Kumkumbuka mwanamke huyu mwenye hekima na mfilosofia wa Iran, sambamba na siku ya kumkumbuka Mulla Sadra, ni fursa ya kupitia upya nafasi ya wanawake mashuhuri katika historia ya kisasa ya Iran, na umuhimu wa kuwa na vielelezo katika sekta ya elimu na maadili ya Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha