Jumatatu 12 Mei 2025 - 13:54
Je! Kwa nini Kiongozi wa Mapinduzi aliunganisha Hawza na Historia?

Kiongozi wa Mapinduzi katika ujumbe wake kutokana na mnasaba wa kutimia miaka mia moja tangu kuanzishwa upya kwa Hawza ya Qom, kwa kusisitiza nafasi kuu ya historia katika uelewa wa dini, alikumbushia kwamba: "Kuutambua Uislamu bila kuelewa historia haiwezekani." Ujumbe huu, kwa kuchambua uhusiano kati ya kutawaliwa na fikra za kielimu na kutengana na uhalisia wa jamii, uliangazia ulazima wa wanazuoni wa kidini kuwa na maarifa yanayo endana na wakati.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Alireza Panahian katika makala yake kuhusiana na ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu alio utoa kwa mnasaba wa miaka mia moja tangia kuanzishwa upya kwa hawza ya Qom aliandika:

Kwa nini Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi alianza tamko lake kwa kutaja historia ya hawza ya Qom?

Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi alianza tamko lake muhimu kuhusu hawza ya Qom kwa utafiti mzito wa kihistoria; yaani, badala ya kusema kwa urahisi kuwa miaka mia moja iliyopita hawza ya Qom ilianzishwa upya na kisha kuingia kwenye maana ya hawza, elimu ya kidini, na majukumu ya mwanazuoni wa dini, kwanza aliashiria mazingira ya kihistoria ya kuzaliwa kwa hawza, si tu ndani ya Iran, bali katika ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.

Katika utafiti kuhusu historia ya kuanzishwa upya kwa hawza ya Qom, mara chache huwa wanazuoni wa dini huakisi juu ya mazingira ya kihistoria ya kuzaliwa kwa taasisi kama hawza katika eneo hili. Hii inatokana na haiba ya kifikra ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ambaye ni mwenye mwelekeo mkubwa wa kihistoria, na hali hii ya kuzingatia historia inaonekana wazi katika hotuba zake nyingine, hata katika maelezo yake ya kidini kabla ya mapinduzi akiwa mjini Mashhad.

Huenda tunapaswa kukuza zaidi sehemu hii ya mwanzo ya barua hiyo na kuyatoa kwa kina yale ambayo hayakupata nafasi katika muhtasari wa barua, na kuyasambaza kwenye jamii. Kuelewa ukubwa wa hawza ya Qom, na kwa ujumla hawza zote za Kiislamu, si jambo linalowezekana bila ya kuzingatia nafasi na mchango wake wa kihistoria.

Kumtambua Uislamu bila ya kuitambua historia ipasavyo, haiwezekani

Katika Barua ya 31 ya Nahjul Balagha, Amirul-Mu’minin (a.s.) alimwelekeza kijana aliyekuwa akimzungumzisha kuzitazama historia. Barua hii, ambayo kimsingi ni kijitabu cha kwanza cha mafunzo ya kidini katika historia ya Uislamu, licha ya kuwa yeye (a.s.) alikuwa na uunganisho wa moja kwa moja na Wahyi, na chochote atakachokisema bila hata ya rejea ya kihistoria ni hoja ya kisheria kwa ajili yetu, bado alisisitiza historia kwani yeye pia anahusiana moja kwa moja na ukweli wote wa ulimwengu.

Katika Qur’ani Tukufu pia, mara nyingi Menyezi Mungu Mtukufu amesisitiza kusoma historia na habari za waliotangulia, na aya nyingi za Qur’ani ni masimulizi ya Mitume, na hata historia ya mataifa, ambapo kwa mujibu wa Allama Tabataba’i (q.s.), uwasilishaji wa historia ya mataifa ni miongoni mwa ubunifu mahsusi wa Qur’ani.

Zingatio la msingi kwa historia katika mchakato wa fiqh ni jambo la lazima, na tunapaswa kuweka misingi ya kielimu na mbinu madhubuti za kunufaika zaidi na historia katika uwanja wa fiqh. Mara nyingine, kuelewa hukumu moja ya Kiislamu iliyopokelewa katika riwaya inategemea kabisa uelewa wa wakati ambao kauli hiyo ilitolewa imekuwa katika mazingira gani.

Tunawezaje kutaka kuutambua Uislamu bila ya kuelewa historia yake? Kuutambua Uislamu bila ya kuielewa ipasavyo historia ya Kiislamu haiwezekani. Wakati mwingine mtu anaona baadhi ya wanazuoni wanatoa maoni kuhusu masuala ya kisiasa, kijamii, na mitazamo ya kidini. Unapozungumza nao kwa karibu, unagundua kuwa ama hawana hata chembe ya uelewa wa historia, au kama wanajua historia, hawajaichunguza kwa ukamilifu na kwa upana.

Historia ni kile ambacho Maimamu wa uongofu (a.s.) walikitunza kwa kutoa shahada na kuuawa kwa ajili yake.

Historia ni kile ambacho Maimamu wa uongofu (a.s.) walikitunza kwa kutoa shahada na kuuawa kwa ajili yake. Maimamu (a.s.) ndani ya historia waliiwekea historia alama kwa shahada zao; waliweka athari yao katika nyoyo za wapenzi wao ndani ya muktadha wa kihistoria. Sherehe hizi za kuzaliwa kwa Imam Ridha (a.s.), na maadhimisho ya kuzaliwa kwa Maimamu wa uongofu (a.s.) yanamaanisha nini? Ni mjadala wa kihistoria. Baada ya muda mfupi tutaadhimishaa kumbukumbu ya shahada ya Imam Jawad (a.s.). Waumini hukusanyika na kuzungumza kuhusu mitihani ambayo wafuasi wa Ahlul Bayt walipitia katika kipindi cha kuzaliwa na uongozi wa Imam Jawad (a.s.). Haya yote ni vipengele katika historia.

Imamu Khomeini (r.a.) alisema: “Sasa hivi ni miaka elfu moja na mia nne ambapo kwa minbari hizi, kwa maombolezo haya, kwa misiba hii, na kwa kupiga vifua vifua hivi, wametuhifadhi; hadi leo wametufikishia Uislamu.” Kisha akaongeza: “Ni maombolezo yaliyohifadhi minbari hii. Kama maombolezo haya yangalikosekana, basi minbari hii nayo isingekuwepo, wala maudhui haya yangalikosekana. Maombolezo haya ndiyo yamehifadhi.” Maombolezo hayo ndiyo kiini halisi cha historia; msingi wa historia, sehemu yake yenye gharama kubwa zaidi.

Kwa nini kuelewa jukumu la sasa na la baadaye la hawza hakuwezekani bila ya kuelewa historia?

Sasa tunataka kuelewa jukumu letu la kihistoria ni lipi? Tunapaswa kuwa wenye maarifa ya wakati, na hili linahusiana moja kwa moja na uelewa wetu wa historia. Tukiwa hatujatambua hili, tunaweza kufanya mambo mazuri elfu moja ambayo hayahusiani kabisa na jukumu letu la kihistoria, kwa sababu wakati uliopo ni wa aina tofauti, kwani muda huwa katika hali ya kubadilika na kugeuka daima. Na katika zama zetu, kuliko wakati wowote ule, hali zinabadilika kwa kasi kubwa zaidi.

Maarifa ya wakati hayawezekani bila ya maarifa ya kihistoria. Hayo maarifa ya wakati ambayo Mtume (s.a.w.w) alisema:

«الْعَالِمُ بِزَمَانِهِ لَا تَهْجُمُ عَلَیْهِ اللَّوَابِس‏»

yaani, mwanazuoni anayeijua zama zake haandamwi na mkanganyiko.

Maana yake ni kuwa mtu ambaye hajui zama zake si kwamba tu atakosea mara chache, bali atadhihirika kwa makosa mengi. Maimamu wetu wamesisitiza sana kuhusu ulazima wa kuwa na maarifa ya wakati. Basi sasa tuko katika zama gani?

Haiwezekani kabisa kuelezea jambo sasa hivi bila ya kufahamu historia ya nyuma na hata ile inayotarajiwa mbele. Lakini bila historia, tutasema tu: Naam, sasa hivi kuna machafuko katika eneo. Lakini machafuko hayo hayawezi kueleweka maana yake halisi ni nini. Sasa hivi kuna mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Sasa hivi Shia wamepata nguvu. Sasa hivi Shia wanapitia dhulma mpya. Haya yote hayawezi kueleweka bila ya kutaja historia yake.

Mojawapo ya hoja muhimu za maarifa ya wakati zilizopokelewa kutoka kwa Imam Ridha (a.s.) ni kuwa alisema: "baadhi ya Shia dhaifu" sijui kama alimaanisha dhaifu wa uelewa na basira, au dhaifu wa mali katika zama hizo walitarajia yeye avae nguo za magunia, za bei rahisi na zilizochakaa, na hata tandiko lake liwe duni na lililochoka. Hili ndilo lilikuwa hitaji la baadhi ya wafuasi dhaifu wa Shia. Lakini Imam alisema: sasa wakati umebadilika, na haiwezekani tena kuishi kwa namna ile ile.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha