Jumatatu 27 Januari 2025 - 21:58
Jinsi Imam al-Kadhim (a.s) alivyotenda kwa ajili ya Mashia katika zama za ghaibu

Msemaji wa Haram Tukufu ya Bibi wa Karama (Sayyidat Fatima Maasoumah, amani iwe juu yake) alisema kwamba Imam Kadhim (amani iwe juu yake) alisema: “Wamebarikiwa Mashia (Wafuasi) wetu ambao wana mapenzi kwetu katika Enzi ya Kutokuwepo kwetu (zama za ghaiba yetu); Wamesimama imara katika kutufuata na wanaepuka chochote chenye harufu ya kwenda kinyume na sisi na upinzani kwetu), amesema: Kwa ajili ya zama za ghaibu, Imam Mussa Al_Kadhim (a.s) alitoa Njia ya utendaji na akasema: Mashia ni kama watu wa Bani Israil, ambao waliomba faraja toka kwa Mwenyezi Mungu, wanamuomba Mwenyezi Mungu Faraja ya Imam wa Zama (a.t.f.s), na Mwenyezi Mungu anawafikishia na kuwaletea Faraja ya Imam wa Zama (a.t.f.s).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hojjatul-Islam wal-Muslimeen Syed Hossein Muumini alisema katika Sherehe ya Shahada ya Imam Kadhim (amani iwe juu yake) katika Haram /Madhabahu Takatifu ya Bibi wa Karama, kwamba hakuna ibada iliyo juu zaidi ya kuwasaidia Masikini. , alisema: Kusaidia wengine ili kukidhi mahitaji yetu wenyewe na kutatua matatizo yetu pia ni jambo zuri sana.

Akisema kwamba kauli za Maimamu Maasumina (amani iwe juu yao) hazikomei (haziishii) kwenye zama na wakati maalum, bali walikuwa wakitoa kauli kwa kutangulizi zama zao na kisha kuzikusudia zama zilizofuata, alisema: Imam Kadhim (a.s) pamoja na yale mateso yote aliyoyaona na kuyapitia kwa miaka mingi ya maisha yake akiwa gerezani, Lakini hawakuwahi kamwe kukosa kuwaongoza watu kuelekea katika Uongofu.

Akizungumzia riwaya ya Imamu Kadhim (amani iwe juu yake) kuhusu Imam Zaman (a.s), msemaji wa Haram Tukufu ya Bibi Mtukufu alisema: Yunus bin Abdul Rahman anasema, nilikuja kwa Imam na kumuuliza, “Je! unasimama (Kuongoza) kwa Haki?" Akasema ndiyo, ni mimi (Kiongozi) katika wakati wangu; Lakini anayesimamia Haki na kuijaza Dunia Uadilifu ni kizazi cha tano cha wanangu ambao wana ghaibu (ghaiba) ya muda mrefu.

Profesa wa Seminari (Hawzat) ya kielimu alisema kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa amepanga miaka 400 ya mateso (adhabu) kwa Wana wa Israeli; Lakini baada ya miaka 230 kupita, kwa sababu walimuomba Mwenyezi Mungu siku 40 mchana na usiku wakikesha na kumuomba Mwenyezi Mungu awape nafuu (faraja), Mwenyezi Mungu akawasamehe na kuwaondolea adhabu ya miaka 170 mingineyo.

Ameeleza kwamba kadiri jina la Imam Zaman (Imam wa Zama) linavyozidi kuwa katika jamii yetu ndivyo jamii inavyokuwa na amani zaidi, alisema: Imamu Kadhim (amani iwe juu yake) aliwasilisha suluhisho (Njia ya utendaji kwa Mashia) kwa Zama za Ghaibu na akasema: “Wamebarikiwa Mashia (Wafuasi) wetu ambao ni wenye mapenzi kwetu Sisi katika Zama za Ghaibu, na wanatufuats Sisi kwa uimara na kujiepusha na chochote chenye harufu ya upinzani kwetu (kinachopingana na) Sisi Ahlul-Bayt. Watu hawa ni Mashia wetu na pia tunawakubali kuwa ni Mashia wetu.

Hojjat al-Islam wal-Muslimeen Momini akaendelea: Mtume alisema mara mbili, "Imebarikiwa hali ya Mashia wetu, na ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba Mashia hawa watakuwa na daraja sawa na sisi Siku ya Kiyama."

Akibainisha kuwa Mapenzi yapo chini ya elimu (Mapenzi ni Sehemu ya Maarifa), alisema: Asili ya mtu kuwa Shia (mfuasi wa Ahlulbayt a.s) kunatokana na mambo makuu matatu ambayo ni: Elimu (Maarifa), Mapenzi na Utiifu, na ikiwa vitatu hivyo vipo ndani ya Nafsi ya mtu, basi mtu huyo atakuwa ni Shia wa kweli na hakika.

Msemaji wa Madhabahu / Haram Tukufu ya Bibi wa Karama alisema: Ahlul-Bayt (a.s) ni watu wenye kuwashika mkono Wafuasi / Mashia wao na ni Watoto wa Mama ambaye, katika dakika zake za mwisho wa Uhai wake, alimuomba Mwenyezi Mungu awasamehe wakosefu wa Umma wa Baba yake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha