Alhamisi 20 Agosti 2026 - 10:48
Hadithi ya Leo | Ubora na Thamani ya Mtoto wa Kike

Hawzah/ Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) katika hadithi moja ameeleza kuhusu nafasi yenye thamani juu ya mabinti wanao jistiri na kujihifadhi pamoja na thawabu ya kuwa nao.

Shirika la Habari la Hawza, limechapisha hadithi ifuatayo kutoka katika kitabu kiitwacho Makarim al-Akhlaq.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww) amesema:

«نِعمَ الوَلَدُ البَناتُ المُخَدَّراتُ، مَن كانَت عِندَهُ واحِدَةٌ جَعَلَهَا اللّه ُ سِترا لَهُ مِنَ النّارِ، وَمَن كانَت عِندَهُ اثنَتانِ أَدخَلَهُ اللّه ُ بِهِمَا الجَنَّةَ ، وَإِن كُنَّ ثَلاثا أو مِثلَهُنَّ مِنَ الأخَواتِ، وَضَعَ عَنهُ الجِهادَ وَالصَّدَقَةَ.»

“Bora ya mtoto ni mabinti wenye kujisitiri na kuwa na haya! Mwenye kuwa na binti mmoja, Mwenyezi Mungu humfanya binti huyo kuwa stara kwake dhidi ya Moto. Na mwenye kuwa na mabinti wawili, Mwenyezi Mungu kwa sababu yao humuingiza Peponi. Na ikiwa ana mabinti watatu, au idadi kama hiyo miongoni mwa ndugubwa kike, Mwenyezi Mungu humwondolea wajibu wa jihadi na sadaka [ya mustahabu].”

Rejea:
Makarim al-Akhlaq, Juzuu ya 1, uk. 472, Hadithi ya 1613; Rawdat al-Wa‘idhin, uk. 404.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha