Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sheikh Ali Al-Khatib, Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia nchini Lebanon, wakati wa hotuba yake katika hafla ya kumbukumbu ya siku ya saba ya Shahidi Ali Al-Khatib, iliyofanyika katika mji wa Labaya, eneo la Biqa‘ Magharibi, alisisitiza kwamba; wanachotaka kwetu ni kujisalimisha, jambo ambalo linatupeleka kwenye maangamizi. Alieleza kuwa kuna njama ya ndani, ya Kiarabu na ya kimataifa inayolenga kuuangamiza Muqawama kwa manufaa ya utawala wa Kizayuni.
Sheikh Al-Khatib alisema: Tunaamini kwamba; dunia hii ni nyumba ya majaribio, mitihani na utekelezaji wa imani za mwanadamu, leo sisi sote tuko katika mtihani; mataifa hupimwa wakati wa shida na mazingira magumu, si wakati wa ustawi na raha, bali katika majukumu makubwa na matatizo.
Tunapoombwa tuyatoe kafara maisha yetu, watoto wetu, wapendwa wetu na mali zetu, ndipo tunapokuwa katika mtihani; je, tunachagua njia ya usalama na kujisalimisha, au njia ya shahada, kujitolea, heshima na utu? Yeyote anayejisalimisha, licha ya kujisalimisha kwake, ataendelea kuwa duni na mwenye kudhalilika; lakini anayechagua njia ya kujitolea, amechagua njia ya heshima na ushindi, na atakuwa mwenye heshima na mshindi.
Watu wanashangazwa nanyi, na kujitolea kwenu, subira yenu, msamaha wenu na jihadi yenu; mshangao huu hauhusu tu yule anayeitoa damu yake, bali pia yule anayevumilia mateso, anayeondoka nyumbani na katika ardhi yake ili arudi akiwa na heshima na ushindi, hii ndiyo tofauti kati yenu na wengine.
Aliongeza kusema: Mbali na hatari mnazokabiliana nazo na kukabiliana na adui Mwisraeli, ikiwa ni pamoja na kujitolea, kuwapoteza wapendwa, kuharibiwa nyumba na kuhama makazi, wanauliza: Lengo la jihadi hii na kujitolea huku ni nini? Wanawaambia mchague njia nyingine: njia ya kujisalimisha. Lakini kujisalimisha mbele ya adui huyu maana yake ni kuelekea kwenye maangamizi, kwa sababu yeye ni adui wa uhai.
Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia aliendelea kusema: Tuna mifano ndani ya Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu; matokeo ya makubaliano ya kujisalimisha kwa adui Mwisraeli yalikuwa nini? Hakuna hata moja kati yao iliyotekelezwa.
Leo tunasikia kwamba waziri mkuu wa adui anasema hatatoka Ghaza na hatatekeleza makubaliano yanayoitwa “makubaliano ya amani” huko Ghaza. Atatekeleza makubaliano hayo kwa sharti moja tu, nalo ni Muqawama na Hamas kunyang’anywa silaha; na ikiwa, Mungu aepushe mbali, Hamas na Muqawama nchini Palestina vitakabidhi silaha zao, watawachinja.
Wapalestina walikuwa na uzoefu kabla ya mwaka 1947; wakati walipowashinikiza watu wa vijiji vya Palestina kukabidhi silaha zao, walifika katika vijiji hivyo na kuanza kuua umati wa watu wa Palestina.
Alisisitiza: Tuna uzoefu mwingi na adui huyu, si uzoefu mmoja tu. Uamuzi wa 1701 wa mwaka 2024 ulikuwa na matokeo gani? Hakuna chochote kilichotekelezwa na mashambulizi yaliendelea, kiasi kwamba katika kipindi cha miezi 15, mashahidi 500 walianguka.
Sasa, kwa madai kwamba usitishaji mapigano umeanzishwa, usitishaji huo wa mapigano uko wapi? Uharibifu na kusafishwa vijiji ambavyo adui amevikalia kwa mabavu, kuanzia Khiyam hadi Naqoura, kunaendelea, na haujaacha kijiji chochote. Vijiji hivyo, ambavyo zamani vilikuwa vimejaa watu na majengo, adui amevigeuza kuwa majivu kwa mabomu yake usiku na mchana.
Sheikh Al-Khatib aliendelea kusema: Serikali hii ya Lebanon ilisema kwamba itaingia katika mazungumzo ya moja kwa moja ili kutuletea usalama na amani, kuanzisha usitishaji mapigano na kufanikisha uhuru, ili watu wa ardhi hii warudi katika nyumba zao, lakini matokeo yalikuwa nini?
Matokeo yalikuwa kwamba utawala wa Israel, siku iliyofuata baada ya kusainiwa kwa makubaliano, ulisema kwamba hautaondoka katika maeneo hayo na umeamua kujenga vituo vikubwa vya kijeshi ndani yake, na kuyatangaza maeneo hayo kuwa maeneo ya usalama kwa ajili ya kufanya ulinzi kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Alisema kuwa: Kwa bahati mbaya, viongozi hawa hawasemi ukweli na hawasemi kwamba adui huyu hana nia ya kutekeleza makubaliano; badala yake, wanamjibu adui kwa kukubali na kumpatia visingizio, kwa nje wanasema jambo moja na kwa ndani jambo jingine.
Baadhi ya viongozi wa vyama ambao wana uadui dhidi ya Muqawama, katika kauli zao au mazungumzo yao na baadhi ya mamlaka, wanasema kwamba hakuna matumaini isipokuwa kupitia njia ya Iran, ili Israel iondoke kusini mwa Lebanon.
Naibu Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Kiislamu la Mashia alisema mwishoni: Tangu mwanzo tuliwaambia kwamba njia mnayofuata kwa hakika inaleta madhara, nanyi mkasema kwamba hamuitaki Iran na kwamba mnataka kukaliwa kwa mabavu, na kwamba hamuitaki Iran.
Je, ardhi hii ni yenu? Je, ninyi mmelipia gharama yake? Sisi, kwa mtazamo wa kihistoria, tumelipa gharama ya ardhi hii.
Ikiwa Iran, katika kukabiliana na adui, itatusaidia kuikomboa ardhi yetu, kama ambavyo imekuwa ikitusaidia katika kipindi chote tangu mwanzo wa mapigano, je, hilo ni haramu? Kwa nini?
Hapa kuna njama ya ndani ya nchi za Kiarabu pamoja na Israel dhidi ya Muqawama huu na dhidi ya watu wa eneo hili.
Maoni yako